Jumamosi, 19 Aprili 2014

WANASIASA WAONYWA JUU YA MADHABAHU




 Baadhi ya viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo  wakiwa katika maombi ya kuliombea Taifa, katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa, moja ya mkutano wa maadhimisho ya PASAKA, ulioandaliwa na kanisa la NEW LIFE IN CHRIST la mkoani Iringa.
 Wakiendelea na maombi ya kuliombea Taifa la Tanzania katika uwanja wa Mwembetogwa manispaa ya Iringa.

 Wakiendelea na maombi.

 Licha ya mvua kubwa kunyesha lakini bado wanaendelea na maombi.

 Eliezely Kamwela - Askofu wa kanisa la Living Covenant la jijini Mbeya akiwa katika uwanja wa Mwembetogwa baada ya kumaliza maombi hayo.
 Askofu Eliezely Kamwela - wa kanisa la Living Covenant la jijini Mbeya, aliyeongoza maombi hayo.
 Baadhi ya waumini wakiwa katika uwanja wa Mwembetogwa mjini Iringa.

 Waimbaji wakisherehesha.



 
 <<<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>>>>
VIONGOZI wa dini kote nchini wametakiwa kuacha mara moja tabia ya kuwakaribisha wanasiasa katika madhabahu ya Mungu  kuhubiri maneno siasa ambayo hayana mlengo wa imani za kidini.

Hayo yamezungumzwa na wachungaji na maaskofu, wakati wa mkutano wa maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka, ulioandaliwa na kanisa la New Life in Christ la mkoani Iringa, ambapo wamesema kuwapa fulsa wanasiasa kuhubiri siasa makanisani ni kuwagawa waumini.


Akitoa maombi kwa waumini wa madhehebu ya kikisto waliohudhuria mkutano huo wa kuliombea Taifa uliofanyika Mwembetogwa mjini Iringa, askofu Eliezely Kamwela kutoka  kanisa la Living Covenant  la jijini Mbeya amesema viongozi wa dini wanapaswa kuachana na tabia hiyo ambayo inapandikiza chuki na fitina kwa waumini.

 
Aidha Kamwela amesema kumekuwa na mmomonyoko wa maadili kwa baadhi ya  viongozi  wakubwa wa vyama na serikali kutumia lugha za matusi, jambo ambalo kanisa lisipoingilia kati kukemea hali hiyo Taifa linaweza kuingia katika machafuko.

Askofu Kamwela amesema baadhi ya viongozi wenye nyadhfa kubwa serikalini wamekuwqa wakitoa Lugha za matusi ambazo haziendani na vyeo walivyonavyo, jambo ambalo linaweza kusababisha tatizo kubwa kwa Taifa na vizazi vijavyo.

"Unakuta mwingine anatukana lakini ni kiongozi mkubwa, Dokta, Profesa au mwanasheria ...lakini kinachotoka kinywani mwake hakitambulishi kuwa yeye ni nani mbele ya jamii, wabunge wanatukanana matusi ya nguoni, jamani Taifa hili linakwenda wapi, watoto wadogo wanaosikiliza au kuangalia Luninga  watachukua nini kutoka kwetu, ndugu zangu tusiwe tunapiga kampeni ambazo hazina macho,  kwani kesho vitu hivi vitatuletea taifa la wapumbavu," Alisema.

Amewataka waumini waelekeze nguvu ya maombi yao kwa mwenyezi Mungu ili  kudhibiti hali hiyo, kwa madai kuwa silaha pekee ya matatizo hayo ni kumshirikisha Mungu kwa njia ya sala katika kukemea viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Naye mchungaji Ezra Kyando katibu  wa Kanisa hilo la New Life la Iringa amesema madhara ya viongozi wa madhehebu ya dini kuwaruhusu wanasiasa kuzungumzia siasa makanisani ni njia ya kuwagawa waumini na kusababisha matabaka.

"Viongozi wa dini wanaowakaribishi  wanasiasa ni makosa makubwa, maana  wanasiasa wanazungumzia siasa ya nchi na wanadini tunazungumzia imani za watu, na ukimkaribisha mwanasiasa kwenye kanisa au msikiti wako inamaana unalenga itikadi ya chama fulani ndani ya kanisa lako, na wakati mwingine inaweza kutokea mavurugano kwenye Makanisa au misikiti," alisema.

Gideon Mwakalinga wa kanisa la New Life amewataka wananchi na waumini wa dini mbalimbali kutanguliza maombi zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu, ili nchi iwe na amani na utulivu, kwa madai kuwa maombi ni silaha ya kila lililo ovu.
MWISHO





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni