Jumapili, 6 Aprili 2014

WAVUNAJI SAOHILL WAIJIA JUU SERIKALI


 Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu (Katikati) akiwa na meneja wa Shamba la msitu wa Saohill Salekh Beleko (Mwenye suti nyeusi) na kulia ni Mwenyekiti wa wavunaji Christian Ahia wakisikiliza jambo katika mkutano huo wa wavunaji uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi- Iringa.
 Baadhi ya wavunaji wa Shamba la msitu wa Saohill wakiwa katika mkutano huo.
 Baadhi ya wavunaji wakiwa katika mkutano huo wa kugomea utaratibu mpya wa ugawaji wa vibari kwa utaratibu wa mnada.
 Meneja wa Shamba la msitu wa Saohill Salekh Beleko na mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu wakisikiliza michango ya wavunaji.
 Mmoja wa viongozi wa wavunaji wa Shamba la msitu wa Saohill Mufindi (Kulia) akiwaza juu ya utaratibu huo wa mnada. Kulia ni Salekh Beleko meneja wa shamba, wakiwa katika mkutano wa wavunaji.
 Manufaa ya Msitu wa Sao hill- ni gari lililotengenezwa kwa Mbao na mmoja wa wadau wa msitu wa Saohill Bw. Kenned Mwangoka.
 Bw. Kenny .. akiwa katika usukani wa gari lake hilo la Miti, ambalo nila pili tangu aanze ubunifu huo, na sasa amepewa tenda na rais wa Botswana mfalme Mswati kutengeneza gari la Mbao kama ni sehemu ya kudumisha Utalii nchini Botswana
 Bw. Kenny Mwangoka mmoja wa wadau wa shamba la msitu wa Saohill na mbunifu wa magari ya mbao Wilayani Mufindi- Iringa akiteremka katika gari lake hilo aina ya Hiace, lenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 10.
 Mmiliki wa Mtandao huu, Bi Oliver Motto akishuhudia usafiri wa Mbao wenye uwezo wa asilimia 100 sawa na aina ya gari halisi hiyo aina ya Hiace.

<<<HABARI >>>
WAVUNAJI wadogo wa miti, katika shamba la Taifa la Sao hill lililopo Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, wamesema msitu huo wa Taifa upo hatarini kuteketezwa kwa moto, endapo  serikali itasimamia msimamo wake wa kuendesha zoezi la utoaji vibari kwa njia yamnada.

Wakizungumza katika mkutano wa kuligomea suala hilo la mnada, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, wavunaji hao wamesema utaratibu wa mnada utawafanya wao wavunaji wadogo wakose fulsa ya kupata vibali hivyo na hivyo kuwa mashuhuda wa wenye fedha wakinufaika na rasilimali hiyo.

Wavunaji hao wameipinga serikali kutumia njia hiyo, kwa madai kuwa itaufanya msitu huo uteketezwe kwa moto, kwani hakuna mwananchi wa Wilaya hiyo atakayekubali kuona rasilimali hiyo ambayo ardhi yake imetolewa na wazazi wake ikiwanufaifa watu wengine tena kutoka nje ya Wilaya ya Mufindi na mkoa wa Iringa.

Francis Bange amesema hawaoni sababu ya serikali kukurupuka na kuanzisha utaratibu huo ambao wao kama wadau wakuu wa msitu huo hawajashirikishwa wala hawafahamu maana na umuhimu wa utaratibu huo, ambapo ameiomba serikali iwahusishe wananchi katika mipango na mikakati yake yote ya shamba hilo.

Apollo Mahenge yeye ameiomba serikali itoe elimu kwanza kwa wananchi juu ya taratibu hizo mbili, Mnada na utoaji wa vibari utaratibu wa kawaida uliozoeleka na wananchi wote, kuliko kuwalazimisha kuingia katika mfumo wa mnada ambao hawajatambua umuhimu, hasara, uzuri hata ubaya wake.

“Hatufahamu maslahi wala athari za mnada, hatuwezi kukikubali kitu ambacho hatukifahamu, tungeiomba serikali itufafanulie ili tuweze kupima kati ya mnada au vibari, kwani hatuwezi kukubaliana na jambo ambalo hatujui umuhimu, manufaa, uzuri, ubaya  wala faida zake,” Walisema.

Matekeleza Mwachang’a amesema haoni sababu ya serikali kukikmbilia utaratibu huo wa kujiongezea mapato na kumsahau mwananchi wa Mufindi ambaye ndiye mtoaji wa ardhoi hiyo bure kwa serikali.

Mwachang’a amesema yeye kama mvunaji mkongwe katika shamba hilo na mlinzi mkuu hakubaliani na utaratibu huo ambao hata wananchi wenye shamba lao hawajajulishwa, huku watu wasionacho wakitengwa na waliokuwa nacho wakibebwa na serikali kupitia mpango huo wa mnada.

Amesema kila mvunaji mmoja ametoa ajira isiyopungua ya watu 14 katika kazi hiyo ya uvunaji, usombaji, upakiaji, ulinzi na upasuaji, na endapo wavunaji wataikosa fulsa hiyo ajira zaidi ya elfu 14 itakosekana na hivyo kuibuka kwa matukio ya uharifu katika Wilaya hiyo.

“Leo tunapozungumzia suala hili la mnada naliogopa sana jambo hili, ninawananchi wengi niliowaajiri ninaisaidia serikali kutoa ajira, hawa wote nitawapeleka wapi, na watafanya kazi gani baada ya sisi wavunaji wao kunyang’anywa hii haki ya kumiliki shamba an kupewa wenye uwezo mkubwa wa fedha,” Alisema Matekeleza.

Godfrey Mosha mmoja wa wavunaji wa msitu huo amesema utaratibu unaotaka kuanzishwa na serikali haujawashirikisha wananchio na hata wadau wa msitu huo, jambo ambalo linaweza kuzua utata mkubwa katia ya wenye ardhi “wananchi”  na wadau wa msitu huo.

Mosha amesema uuzwaji wa vibali kwa njia ya mnada itapandisha gharama za zao la misitu na hivyo wananchi kushindwa kujikwamua kujenga nyumba bora kwa kushindwa kumudu gharama za ununuaji wa mbao, na kuwa maamuzi yaliyofikiwa na serikali hayakuwaangalia zaidi wananchi.

Pia amesema msitu huo kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa ni sehemu ya ajira wanayoitegemea, kwani umetoa zaidi ya ajira milioni 14 kwa watanzania, na mpango huo wa BRN katika Wizara hiyo ya maliasiri na utalii kupitia idara yam situ huo haijawatendea haki wananchi, kwanio itawakandamiza zaidi na hivyo Falsafa ya “maisha bora kwa kila Mtanzania” itakwama.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve, amesema uuzwaji wa vibali kwa njia hiyo ya mnada utaongeza tatizo kubwa la wananchi kutokuwa na ajira na hivyo kuibuka kwa wimbi la matukio ya uharifu, kutokana na asilimia kubwa watu wa Mufindi kutegemea msitu huo kiuchumi.

Mwenyekiti wa wavunaji wadogo wa msitu huo wa Saohill Christiani Ahia, amesema utaratibu huo utawafanya wananchi wa Wilaya ya Mufindi kutokuwa na manufaa na msitu huo, kwa  wakibaki kuwa walinzi na wazimaji wa moto pasipo kupata manufaa yoyote, jambo ambalo ni hatari kwa serikali.

“Taratibu za uvunaji wa misitu ya Saohill ndizo zilizotuchelewesha sisi wavunaji wadogo tushindwe kuingia katika ushindani katika mnada mpaka sasa ni masikini, kwani taratibu zilizopo zimetubana mpaka sasa ni masikini, Sisi watu wa Mufindi ni wastaarabu sana kwa Serikali, hatujawahi kufanya vurugu hata sikumoja, tumeilea huu msitu kwa miaka zaidi ya hamsini, tufaidike jamani!!,” Alisema Tweve.

Aidha ameongeza kuwa… “Serikali ndiyo imetufanya wananchi wa Mufindi tuwe masikini siku zote, lakini leo inapokuja na mpango huu wa Mnada inalenga kutunyang’anga haki ya kunufaika na msitu wetu, kwani hapa hakuna atakayeweza kushindandna na wenye fedha watakaokuja kununua msitu huu,” Alisema Tweve.


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu aliyehudhuria mkutano huo, amesema hana taarifa rasmi za kuanzishwa kwa mpango huo wa mnada, kwa kuwa ofisi yake haijapokea  barua yoyote juu ya utaratibu huo mpya.

Meneja wa Shamba la Saohill Salekh Beleko amekiri kuwepo kwa mpango huo, na kuwa chanzo cha uanzishwaji wa utaratibu huo katika Wizara ya maliasili na utalii ni Wizara ya fedha ambayo ilihitaji kwenda haraka katika mpango wa Matokeo makubwa sasa yaani Big Result Now BRN.

Beleko amesema mpango huo uliingia kwa dirisha la wizara ya fedha ili kuiwezesha serikali kukusanya mapato kwa wingi, ambapo Wizara ya maliasili  na utalii ilionekana inafanya biashara ya wanyama na misitu.

“Sisi tumeingia kwa dirisha la wizara ya fedha ili kuleta matokeo makubwa sasa na ilionekana mnada ndiyo suluhisho, na haikuwa sehemu yote yam situ bali ni sehemu ya misitu asilimia 70 ya mazao yanayotarajiwa kuuzwa yauzwe kwa mnada, na asilimia 30 yauzwe kwa njia ya kawaida,” Alisema Beleko.

Aidha Beleko amesema serikali baada ya kutambua umuhimu wa wananchi wake katika kuutegemea msitu huo, ilifanya mageuzi kwa kubadili asilimia 70 iuzwe kwa njia ya kawaidda ya utoaji wa vibari, huku asilimia 30 ikitakiwa iuzwe kwa njia ya mnada.
MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni