Jumatatu, 7 Aprili 2014

WASANII IRINGA WAFANYA KUFURU "KANUMBA DAY"

 T.Shirt za kikundi cha Prince Production cha Iringa mjini, zilizovaliwa katika siku ya "Kanumba Day", kama ni sehemu ya kumuenzi marehemu Kanumba, ambapo wasanii wa kikundi hicho cha Prince Production kiliweza kuwatembelea wagonjwa na kutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
 Mackdonad Msemwa msanii wa kikundi cha Prince Production akiwa nje ya moja ya Wodi ya wagonjwa kabla ya kuanza kutoa misaada kwa wagonjwa, kama ni sehemu ya kumuenzi msanii Steven Kanumba, ikiwa ni miaka miwili tangu afariki dunia.
Prince Henry akiwa amemnyanyua mtoto katika wodi ya watoto waliolazwa katika Hospitali ya mkoa wa Iringa, ambapo pia kikundi cha wasanii cha Prince Production kimetoa misaada mbalimbali pamoja na kuwajulia hali wagonjwa wa Hospitali hiyo kama ni sehemu ya maadhimisho ya miaka miwili ya kifo cha msanii mwenzao Steven Kanumba "The Great"








Samuel Manumba, msanii wa sanaa ya maigizo mkoani Iringa, akiwa nje ya Hospitali ya mkoa wa Iringa kabla ya kuingia katika word mbalimbali kuwaona wagonjwa.
 Wasanii wakitoa baadhi ya misaada kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kama ni sehemu ya kumuenzi Steven kanumba, kutimiza miaka miwili tangu afariki dunia.
  Wasanii wakitoa baadhi ya misaada kwa wagonjwa wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, kama ni sehemu ya kumuenzi Steven kanumba, kutimiza miaka miwili tangu afariki dunia.


 Wasanii wakiwa na wagonjwa hospitali ya mkoa wa Iringa.


Magreth Mfikwa akiwa wasanii wa kikundi cha Prince Production Kushoto ni mkurugenzi wa kampuni ya Prince katikati ni  Samwel Manumba na kulia ni Mackdonad Msemwa

<<<HABARI>>>

KATIKA kumuenzi marehemu Steven kanumba wasanii wa sanaa ya maigizo mkoani Iringa, wameitumia siku hiyo ya kumbukumbu ya kifo cha msanii Steven Kanumba kwa kufanya shughuli za kijamii, ikiwa pamoja na kuwatembelea wagonjwa na kutoa misaada mbalimbali .

Wasanii hao wamesema Kanumba alikuwa ni kioo sahihi katika jamii, na kamwe mambo aliyoyafanya hayawezi kufutika katika mioyo ya Watanzania, kwani  aliweza kuyasaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji.

Prince Henry mratibu wa “Kanumba Day”kutoka kikundi cha Prince Production cha mkoani Iringa amesema wameamua kumuenzi msanii mwenzao kwa kufuata nyayo zake alizokuwa akizifanya, ili kuyaendeleza matendo yake mema katika jamii.

Henry amesema ipo haja kwa wasanii wote nchini kutenga siku hiyo ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba kwa kufanya shughuli za kijamii ili kuyaendeleza yale mema aliyoyapanda katika mioyo ya Watanzania.

“Kanumba The Great alikuwa ni kioo sahihi kwetu wasanii na jamii kwa ujumla, ni mfano mzuri wa kuigwa, kwani hata leo haya tunayoyafanya ni msukumo wa yale mema aliyoyafanya kwa makundi mbalimbali yenye uhitaji kama wagonjwa, watoto yatima na walemavu, na sisi kama wasanii wa Iringa tumeona tukumbuke matendo yake kama ni sehemu ya kuomboleza kifo chake,” Alisema Henry.

Mackdonald Msemwa msanii wa kikundi cha Prince Production naye amesema umuhimu wa siku hiyo ndiyo imewafanya kuwatembelea wagonjwa, kwani hakuna msanii mwenye sifa zinazofanana na marehemu Kanumba.

Swabra Juma amesema wameamua kuwatembelea wagonjwa hasa katika wodi muhimu za akinamama na watoto ili kuiendeleza mbegu aliyoipanda Kanumba ya kujitolea katika jamii jambo ambalo limeweka dira isiyofutika katika mioyo yao.

Samwel Manumba wao kama wasanii mkoani Iringa, wanaopaswa kudumisha utamaduni huo ambao ulianzishwa na  muasisi wao Steven Kanumba.

"Kanumba alikuwa ni mtu wa kujichanganya katika jamii kwa kutoa misaada mbalimbali na hata kuwatembelea wagonjwa, yatima na watu wote wenye shida, leo hii mioyo yetu imeguswa kuyafanya yale aliyokuwa akiyafanya Kanumba, ni sawa ametutoka lakini ndani ya nafsi zetu bado anaishi na yupo hai,” alisema. Samweli Manumba.

Rehema Madawili na Sophia Kalopo baadhi ya wagonjwa waliopatiwa msaada huo wamewashukuru wasanii hao ikiwa pamoja na kuwaasa wasanii hao kuwa na umoja katika matatizo mbalimbali kwa lengo la kukuza tasnia ya sanaa nchini.

Hata hivyo Magreth Mfikwa mama aliyejifungua watoto watatu mapacha siku ya Kanumba, amesema kwake yeye ni siku ya furaha kuwapata watoto hao, huku akiitaka jamii kuithamini taaluma ya sanaa na kuona ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Magreth amejifungua watoto mapacha watatu, wawili wakiwa watoto wa kike na mmoja wa kiume, ambapo mama wa watoto hao amesema mtoto huyo wa kiume atampatia jina la Steven ili kuenzi siku ya kumbukumbu ya kifo cha Kanumba.

Nao uongozi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa kupitia muuguzi mkuu Onolatha Mbwelwa amesema wasanii wote nchini wanapaswa kuiga mfano huo wa wasanii wa Iringa, kwani suala hilo limeonyesha upendo juu ya msanii mwenzao Kanumba aliyekuwa ni kipenzi cha watanzania katika tasnia hiyo ya filamu.
MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni