Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono wa shukrani na Lambardo Mvanda, mwakirishi wa timu ya Black Cheeter ya Iringa mjini- wakati timu zinashiriki Kombe la Muungano zilipopatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono wa shukrani na Maulid Mwanyange,
mwakirishi wa timu ya Mucoba Kids.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonce akipeana mkono Mose Masas,
mwakirishi wa timu ya Incomet VTC FC ya mjini Mafinga- wakati timu
zinashiriki Kombe la Muungano zilipopatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na
mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
Akipokea Mpira, jezi na soksi.
Mwakirishi wa timu ya Mbeya City ya jijiji Mbeya- Dotto Sanga- akipokea jezi ya timu yake, mara tu baada ya timu
zinashiriki Kombe la Muungano kupatiwa msaada huo wa jezi seti 6 na
mipira kumi na kampuni ya Chai Bora.
Soud Mlindwa
mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya, timu iliyochukua ubingwa wa kombe hilo la Muungano, akipokea jezi na mpira kutoka kwa mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.
Soud Mlindwa
mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya, timu iliyochukua
ubingwa wa kombe hilo la Muungano, akipokea mpira kutoka kwa
mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.
Shukuru Millinga - mwakirishi wa timu ya Zamaleck ya mjini Njombe, akipeana mikono ya shukrani mkurugenzi wa Chai Bora Petronilla Alphonce.
Mratibu wa mshindano ya "Kombe la Muungano" Daud Yasin, akizungumza na wawakirishi wa vilabu shiriki, mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo- Jezi seti 6 na mipira 10.
Wawakirishi wa timu zinazoshiriki kombe la Muungano, wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chai Bora, pamoja na mratibu wa mashindano hayo Daud Yasin.
Wakiwa katika Picha ya pamoja.
Jane Ndosa- mhasibu wa kampuni ya Chai Bora, akiwa na Dotto Sanga, mwakirishi wa timu ya Mbeya City, mara baada ya timu shiriki kupatiwa misaada na kampuni ya Chai Bora ya Mufindi- Mafinga mkoani Iringa.
Kulia ni Moses Masasi wa timu ya Incomet VTC FC akiwa na mwakirishi mwenzie katika uwanja wa kiwanda cha Chai Bora.
Moulid Mwanyange (Kushoto) mwakirishi wa Mucoba Kids, akiwa na Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya.
Moulid Mwanyange (Kushoto) mwakirishi wa Mucoba Kids, akiwa na Soud Mlindwa mwakirishi wa timu ya Mbaspo Academy ya jijini Mbeya.
Francis Mlowe mwakirishi wa timu ya Igowole Fc (wa kulia) ya Wilayani Mufindi, akiwa na Lambardo Mvanda wa timu ya Black Cheeter ya mjini Iringa.
Kulia ni shukuru Millinga na Francis Mlowe.
Maboksi ya Chai Bora, majani ambayo yalitolewa kwa timu shiriki za kombe la Muungano, hiyo ikiwa ni hamasa kwa wachezaji kutumia kinywaji cha Chai na kuepuka vinywaji vyenye kileo.
Wakisikiliza jambo.
Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni ya Chai Bora.
Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni ya Chai Bora.
Mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Mufindi- Iringa Petronilla Alphonceakizungumza jambo na wawakirishi wa timu zinazoshiriki kombe la Muungano.
Aloyce Mnoga mwakirishi wa Incomet VTC FC akiwa na Francis Mlowe wa Igowole FC wakisikiliza ujumbe kwa makini kutoka kwa mkurugenzi wa Chai Bora- Petronila alphonce(hayupo pichani).
Jane Ndosa mhasibu wa kampuni ya Chai Bora akiwa na Lambardo Mvanda, wakifuatilia jambo katika hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa vya michezo.
<<<HABARI>>>
KOMBE la
Muungano “Muungano Cup” ambalo limeanza kutimua vumbi katika uwanja wa
Igowole katika Wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa limepigwa jeki na kampuni ya Chai
Bora, kwa kupatiwa msaada wa jezi seti 6 pamoja na mipira 10 kwa ajili ya
kuboresha mashindano hayo.
Akikabidhi jezi na
mipira hiyo kwa mratibu wa mashindano hayo ya kombe la Muungano- Daud Yasin,
mkurugenzi wa kampuni ya Chai Bora Petronilla Alphonce, amesema lengo la msaada
huo ni kuyafanya mashindano hayo kuwa na muonekano wa pekee, shughuli iliyofanyika katika uwanja wa Chai Bora mjini Mafinga,.
Petronida
amesema vijana hao wanapaswa kujituma katika michezo ili kuonyesha vipaji na uwezo nyanda za juu kusini, ikiwa pamoja
na kutotumia vinywaji vyenye kileo ili kuwafanya wawe na nguvu imara.
Aidha amesema
misaada hiyo imegharimu jumla ya shilingi Milioni 7.7 na kuwa kampuni kwa kutambua hilo imetoa
msaada huo kwa wachezaji wote, na mchango huo ni katika kuunga mkono mashindano
hayo kwa kuiwakirisha kampuni kwa kiwango cha hali ya juu.
“Kampuni kwa
kuthamini michezo imeona ni vema itoe jezi seti 6 na mipira kumi, vifaa vyenye
thamani ya shilingi Milioni 7.7, .. mchango
huu tulioutoa tunajua una manufaa na utatuletea ushindi mkubwa, niwawaombeni pia
vijana mtumie Chai kwani ina manufaa sana kwenye mwili wa binadamu kwani inachangamsha na inaburudisha, ” Alisema
Petronilla.
Akipokea msaada
huo- mratibu wa mashindano hayo ya Kombe la Muungano Daud Yasin amesema kampuni
ya Chai Bora tangu mwaka 1998 imekuwa ikichangia kwa hali na mali sekta ya
michezo mkoani Iringa, na kuwa ni Kampuni ya kwanza kuyadhamini mashindano ya kombe la
Muungano kwa miaka yote.
Amewataka wachezaji
kuthamini vifaa hivyo kwa ubora wake kwani vina ubora wa hali ya juu, na kuwa
matumaini yake ni vilabu shiriki kufanya vyema ili kuitangaza kampuni hiyo
kupitia michuano hiyo inayozishirikisha timu za mikoa ya nyanda za juu kusini.
Amesema mashindano
hayo ambayo yamezinduliwa Mei 24 katika uwanja wa shule ya msingi Igowole ambapo
mashindano hayo yataendeshwa katika viwanja viwili, kwa maana ya kiwanja cha wambi cha mjini Mafinga
na kiwanja Igowole shule ya msingi,
Uwanja wa
Igowole utachezewa na timu ya Mbeya city ya jijini Mbeya, Zamalek na timu ya
Igowole sekondari,
huku mjini Mafinga katika uwanja wa Wambi kutakuwa na mechi ya timu ya
Benk ya wananchi Mucoba, timu ya chuo cha Incoment na timu ya Black Cheeter ya
mjini Iringa.
Amesema timu ya
Mbaspo ambayo ni mabingwa watetezi waliochukua kombe la Muungano mwaka 2013
wamepewa fulsa ya kuingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali, ambapo
amewataka wapenzi wa soka na mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia vipaji
vya vijana wa nyanda za juu kusini.
Hata hivyo
amesema mashindano hayo yamekuwa na msisimko kwa kuwa yanahusisha vijana walio
na umri chini ya miaka 20, huku akiwataka wapenzi na mashabiki wa nyanda za juu
kusini, kujitokeza kwa wingi kutazama vipaji vya vijana wa nyanda za juu
kusini.
Daud Yasini
amesema kwa mwaka huu niwa mwisho kwake kuratibu
mashindano ya kombe la Muungano kwani anastaafu na kuwa bingwa atachukua Kombe
hilo moja kwa moja, kama ni kumbukumbu kwa timu ya uratibu wake wa mashindano
hayo.
Hata hivyo yasin
amesema mashindano hayo yatakamilika june
11, ambapo fainali ya kombe hilo mchezo wake utakachezwa katika uwanja wa Wambi
wa mjini Mafinga.
Nao wawakirishi wameonyesha tambo zao huku kila mmoja akijikweza kulichukua kombe hilo, huku wakiwaomba wadau kuchangia michezo mbalimbali hasa ya soko ambayo imekuwa na mvuto kwa kundi kubwa katika jamii.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni