Wananchi waliofika na mabango yenye ujumbe mbalimbali, katika uwanja wa Mashujaa, katika mkutano wa hadhara wa UKAWA- Mafinga mjini- katika Wilaya ya Mufindi- Iringa.
Baadhi ya vijana wakiwa katika uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga, katika mkutano wa hadhara wa UKAWA, Wilayani Mufindi Iringa.
Moja ya bango likiwa limeshikwa na mwananchi ambaye hakufahamika jina lake, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mjini Mafinga- Wilaya ya Mufindi Iringa.
Wananchi waliofika na mabango yenye ujumbe katika uwanja wa Mashujaa, katika mkutano wa hadhara wa UKAWA.
Wananchi waliofika na mabango yenye ujumbe katika uwanja wa Mashujaa, katika mkutano wa hadhara wa UKAWA.
Shekh Rajab
Katimba- Mw/kiti wa jumuiya ya maimam Tanzania, akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mashujaa Mafinga mjini- katika Wilaya ya Mufindi - Iringa.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Martine Juju Danda, akizungumza na wananchi katika uwanja wa Mashujaa wa mjini Mafinga- Mufindi Iringa.
Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa Mafinga, wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
<<<HABARI>>>
UMOJA wa katiba
ya wananchi wanaopigania rasimu mpya -UKAWA, ambao viongozi wake wanafanya ziara
ya mikutano katika maeneo mbalimbali nchini, umekutaka na kikwazo kikubwa katika moja ya
mikutano yake mkoani Iringa.
Viongozi wa
UKAWA wakiongozwa na mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba, wamejikuta katika
sintofahamu, baada ya baadhi ya wananchi kutinga katika mkutano huo, huku
wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali ambazo zipo kinyume na Mkutano huo.
Mkutano huo
ambao umefanyika katika uwanja wa Mashujaa wa mjini Mafinga- wilaya ya Mufindi
mkoani Iringa, umekutana na zengwe baada ya kundi la wananchi kuwasili na
mabango yenye ujumbe mbalimbali.
Mabango hayo
ndani ya Uwanja huo yameleta sintofahamu, baada ya viongozi na wafuasi wa UKAWA
waliofika katika uwanja huo kusikiliza viongozi, jambo ambalo limemfanya katibu
wa CHADEMA Mkoa wa Iringa Allen Kilewela kuitaka hadhara hiyo kuimba wimbo wa
Taifa, ili kutuliza vurugu hizo.
Aidha Killewela
aliliomba jeshi la polisi kuingilia kati tatizo hilo, ambalo lilikuwa
linatishia usalama wa wananchi waliofika katika mkutano huo, kwani aadhi yao
ambao hawakuridhika na mabango hayo walijikuta wakirushiana maneno makali huku
baadhi yao wakishikana mashati na kupigana.
“Jamani huu
mkutano ni halali, polisi wako wapi?? Naona kuna vijana wamekuja hapa kwa nia
ya kuvuruga mkutano huu, tunawaomba polisi waingilie kati suala hilo, wananchi
waliokuja hapa wawe ni wale ambao wamekuja kuwasikiliza viongozi na si
vinginevyo,” Alisema.
Hatua hiyo
ilimfanya kaimu mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Taifa Martine Juju Danda kupanda
jukwaani na kutoa onyo juu ya wale wanaofanya vurugu katika mkutano huo.
“Nataka
niwaambie ndugu zangu!!, Usije ukapima uimara wa ukuta kwa kupiga ngumu,
Utaumia, tunawatumia salamu wale waliowatuma, kwamba zoezi lenu halitafanikiwa,
na kama mnataka muondoke salama kama mlivyotoka majumbani kwenu tunawaomba
msikilize tutaelewana, kwani huu ni mkutano wa wananchi wanaotaka kujua nchi
yao ipo wapi na inaelekea wapi,” Alisema Danda.
Naye Shekh Rajab
Katimba- Mw/kiti wa jumuiya ya maimam Tanzania, amesema katika mkutano huo hawahitaji
vurugu, bali wanatoa elimu juu ya umuhimu wa serikali tatu, ambazo zitaondoa
kero za Muungano.
Aidha Shekh Katimba
alisema katika kuijadili Katiba, upo umuhimu wa siasa zikabaki katika
mustakabari wake, kuliko baadhi ya viongozi kuchanganya masuala ya siasa na dini,
huku akiwataka viongozi hao kuacha vitisho kwa wananchi na waumini katika
madhabahu matakatifu.
Katimba amesema
katika mchakato wa katiba, wananchi wenyewe ndiyo wanahaki ya kuamua wanataka Katiba
ipi, na kuwa wananchi hawataki ufisadi, na wao ndiyo wanakataa hali hiyo ya
kujilimbikizia mali watu wachache.
“Sisi tunaukataa
ufisadi, kwani nchi hii siyo maskini bali ni tajiri sana, na utajiri huu
tunataka wanaofaidi wawe ni wananchi wote wa Tamzania na siyo watu wachache
kama ilivyo, na ili kumaliza tatizo hili tuikubali serikali tatu ili kupunguza
hata idadi kubwa ya baraza la mawaziri,” alisema.
Aidha Shekh Katimba
amesema nchi ina rasilimali nyingi kama maji ya kila aina, kama Bahari, mito,
maziwa, madini ya almasi, Tanzanite pamoja na Gesi ambayo ni utajiri mkubwa,
huku akisema nchi ya Tanzania ni mali ya kila mmoja, mwenye dini, asiye na
dini, wasio na vyama na wenye vyama na hata masikini.
Baadhi ya mabango yaliyokuwa
yamebebwa na vijana hao yalikuwa na ujumbe uliosomeka “vijana Mafinga tuna
mashaka na ndoa ya Ukawa, watauza nchi” na bango la waendesha bodaboda
lilisomeka “ Rudisheni posho kwanza mjengoni dodoma.”
Mengine na ujumbe wake kwenye mabano
ni lililowatambulisha wafanabiashara wa sokoni lililosomeka “Mafinga Sokoni,
serikali tatu sio suluhisho la matatizo ya wananchi”, na la wapiga debe Mafinga
stendi lilisomeka “Karume Oyee, Nyerere Oyee, Muungano Saafi.”
Bango la waliojitambulisha kuwa ni
machinga lilisomeka “tunataka serikali inayojali wajasiliamali, sio kujali
matumbo yao”, na lile la wakulima lilisomeka “kilimo kwanza, utaifa kwanza.”
Wakati mabango hayo yakizungushwa
katika mkutano huo muda ambao Profesa Lipumba akihutubia, usikivu ulipotea kwa zaidi
ya dakika 20 baada ya sehemu ya kundi la vijana lililokuwa likimsikiliza
kuelekea upande waliokuwa vijana wenye mabango hayo.
Mmoja wa Polisi aliyekuwa
akiwatuliza vijana hao alisema “Jamani huu ni mkutano halali wa kisiasa, acheni
wenzenu wafanye mkutano wao, yatoeni mabango yenu.”
Akielezea vurugu hizo, Profesa Ibrahim
Lipumba amesema zinafanywa na vijana waliotumwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)
kwasababu ya msimamo wao wa kutaka serikali mbili, tuhuma zilizokanushwa na
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu aliyehojiwa baaada ya mkutano
huo.
“Siamini kama mkutano huu ungekuwa
unahutubiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Taifa Jakaya Kikwete wangekuja na mabango
hayo na kufanya vurugu hizi?”
Hata hivyo baada ya vurugu hizo kutulia, Profesa Lipumba aliruhusu maswali huku akifafanua sababu mbalimbali
zilizosababisha wasusie bunge la Katiba na kuanzisha UKAWA.
Profesa Lipumba alisema milango ya
Ukawa ipo wazi kwa mtu yoyote ndani na nje ya bunge la Katiba, wakiwemo wabunge
na viongozi wa CCM, “Tutafurahi kuwapata wana CCM, tunawakaribisha Ukawa ili
kwa pamoja tushirikiane kupata Katiba inayotokana na wananchi,” alisema.
Winfreda Ngoti mwananchi aliyepata fulsa ya kuuliza swali, aliyesema harakati za kudai serikali tatu hazitakuwa na maana
yoyote endapo matatizo ya wananchi hayatashughulikiwa.
“Watanzania wana matatizo lukuki,
vituo vya huduma za afya havina wataalamu, dawa, wakulima hawapati pembejeo kwa
wakati na bei zake ni kubwa, wafanyabishara wadogo wanabanwa na kukamuliwa
kodi, walimu hawapati mishahara kwa wakati, askari wana mishahara midogo na
wanakula rushwa,” alifafanua.
Katika majibu yake, Profesa Lipumba
amesema hayoyote yatafanyiwa kazi kukiwa na Katiba bora itakayosisitiza
uwajibikaji na uadilifu.
Alisema rushwa na ufisadi vimekuwa
kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya Taifa, katika sekta zote ikiwemo elimu,
afya, kilimo, biashara, miundombinu na sekta nyingine.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni