Jumatano, 21 Mei 2014

"KALENGA WEST PARK" YAINUA KIKOSI CHA POLISI FFU

  Jengo la Hotel ya Kalenga West Park ya Mjini Iringa.
Jengo la Hotel ya Kalenga West Park ya Mjini Iringa.
 Frenk Kaundama (katikati) kaimu mkurugenzi wa Hotel ya Kalenga West park akikabidhi jezi kwa kikosi cha kutuliza ghasia FFU Mkoa wa Iringa.
 Frenk Kaundama (katikati) kaimu mkurugenzi wa Hotel ya Kalenga West park akikabidhi jezi kwa kikosi cha kutuliza ghasia FFU Mkoa wa Iringa.

 Nahodha (keptain) wa timu ya  Polisi FFU Mussa Jackson Ndanzi akisikiliza jambo wakati wa makabidhiano ya jezi za wachezaji wake, katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa polisi mkoa wa Iringa (RPS Ramadhan Mungi).
  Viongozi wa polisi Iringa wakisikiliza jambo wakati wa makabidhiano ya jezi za wachezaji wa timu ya polisi FFU, katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa polisi mkoa wa Iringa (RPS Ramadhan Mungi).
 Mmoja wa kiongozi wa polisi Iringa akisikiliza jambo wakati wa makabidhiano ya jezi za wachezaji wa timu ya polisi FFU, katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa polisi mkoa wa Iringa (RPS Ramadhan Mungi).
 Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea msaada wa jezi kwa timu ya Polisi kikosi cha FFU, msaada uliotolewa na uongozi wa Hotel ya Kalenga West Park Iringa.
 Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea msaada wa jezi kwa timu ya Polisi kikosi cha FFU, msaada uliotolewa na uongozi wa Hotel ya Kalenga West Park Iringa.
 Frenk Kaundana (katikati) akikabidhi msaada huo wa jezi kwa timu ya Polisi kikosi cha FFU- Iringa, kulia ni mkuu wa kikosi cha Polisi FFU SP- Said Abdallah Mnunka, kulia ni nahodha wa timu ya FFU Mussa Ndazi.
 "Zitatusaidia sana" kama anasema nahodha wa timu ya Polisi kikosi cha FFUIringa Mussa Ndazi.
 Wakichagua jezi hizo walizopatiwa msaada na Hotel ya kalenga West park.
 Wakichagua jezi hizo walizopatiwa msaada na Hotel ya kalenga West park.





<<<HABARI>>>

 HOTEL ya Kalenga West Park ya mjini Iringa imeisaidia timu ya Polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kwa lengo la kilabu hiyo kuendelea na michezo ambayo pia inasaidia kuuweka mwili katika hali ya ukakamavu na wenye afya zaidi.

Akikabidhi msaada huo kwa SP- Said Mnunka- mkuu wa kikosi cha -FFU – Iringa, kaimu mkurugenzi wa Hotel ya Kalenga West Park Frenk Kaundama amesema lengo la kuiinua timu hiyo iweze kufanya vizuri.

Tukio hilo ambalo limefanyika katika ukumbi wa Polisi mkoa wa Iringa, huku Kaundama akisema wadau wa sekta ya michezo wanapaswa kusaidia vilabu vyao ili kuinua hali ya uchumi, kwa kuwa timu hizo zinapofanya vizuri na kupanda daraja wageni mbalimbali huingia katika mikoa husika na hivyo wafanyabiashara kunufaika kwa kuuza bidhaa.

Kalenga West Park tumechukua hatua ya kuisaidia timu yetu ya FFU maana hawa ni wadau wetu tunaofanyanaokazi, lakini hii timu ikifikia hatua nzuri kwa kupanda daraja timu kama Simba, Yanga na nyingine kubwa zitakuja mkoanbi Iringa kucheza, ule ugeni utalala na kula katika ofisi zetu na hivyo uchumi utakua,” alisema Frenk Kaundama.

Aidha  Kaundama amesema wao kama wadau wa sekta mbalimbali ikiwemo ya michezo wapo tayari kuchangia vilabu vyenye malengo chanya, kwa lengo la kuutangaza mkoa wa Iringa.

Akipokea msaada huo SP- Said Mnunka- mkuu wa kikosi chaPolisi  -FFU – Iringa, ameushukuru uongozi wa Hotel ya Kalenga West Park kwa hatua hiyo, na kuwa kikosi cha FFU kimedhamilia  kujikita katika sekta ya michezo ili kuborsha mahusiano baina yao na jamii, kwamadai ya kuwa kumekuwa na ukuta unaowatenga na wananchi.

“Askari wetu wanatakiwa kuwa tayari kila wakati,wawe wakakamavu na wanaofanya mazoezi,  na kutokana na hilo tumeanzisha timu ya mpira wa miguu, tukaamua kuwatafuta wadau, na kwa bahati nzuri mzee Kaundama  ameamua kutusaidia jezi za wachezaji wa timu yetu, mimi binafsi nimshukuru sana,” alisema Mnunka.

Aidha amewaomba wadau wengine kuichangia timu hiyo, kwa kuwa kikosi cha kutuliza ghasia FFU ni polisi kama vilivyo vikosi vingine katika jeshi la Polisi, huku akiwataka wadau wasiwatenge na kuwaogopa, na kuwa uanzishwaji wa timu hiyo ni kujisogeza zaidi kwa jamii.

PC Mussa Jackson Ndanzi ni nahodha wa timu ya FFU amesema changamoto ya timu yake ni jezi za wachezaji, ikiwa pamoja na uwanja wa michezo na viatu, na kuwa kwa sasa kanisa katholiki limeamua kuwasaidia uwanja ambao ndiyo wanafanyia mazoezi.

“Napenda kutoa shukrani kwa mzee Kaundama, ameliona tatizo letu, kwani tulipoanzisha timu yetu tumekumbana na mapungufu mengi, mojawapo nilaukosefu wa jezi na viatu kama vitendea kazi, lakini bado tunatatizo la uwanja, uwanja bado ni tatizo, ingawa uongozi upo bega kwa bega na sisi, tunawaomba wadau wasituchoke kwani sie tupo mikononi mwao, tutarudisha fadhira kwa kuonyesha kiwango kikubwa cha mpira tulichonacho, timu yetu ni tofauti na timu nyingine, sawa tunamajukumu ya kulinda amani lakini pia tunalo jukumu la kuutangaza mkoa wetu kupitia michezo.
MWISHO.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni