Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wakiwa katika kikao hicho.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Willium Ntinika akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wilayani Mufindi, akisikiliza jambo kwa umakini mkubwa.
Diwani Efrehem Lukunga akisikiliza jambo kwa umakini katika baraza hilo.
Wa
kwanza kulia ni diwani Ernei Nyeho wa Kata ya Mdabulo, akiwa na diwani
Tasil Mgoda wa kata ya Sao hill Mufindi, wakijadili jambo, baada ya
kutoka katika baraza la madiwani.
Moja ya alama ya "X" ambayo huwekwa na TANROAD kama ni irani ya kuondolewa jengo eneo lenye alama hiyo, alama ambazo zimelalamikiwa na baraza la madiwani Mufindi.
<<<HABARI>>>
BARAZA la
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, limeilalamikia Wakala wa barabara mkoa wa Iringa TANROAD kwa madai
ya kushindwa kujenga barabara kwa
kiwango kinachotakiwa, na hivyo
miundombinu hiyo kulazimika kutengenezwa mara kwa mara.
Madiwani hao
wamesema ujenzi wa barabara chini ya kiwango, unaofanywa na TANROAD kamwe
hauwezi kufumbiwa macho, huku wakiitaka mamlaka hiyo kuwashirikisha wataalamu
wa Wilaya husika katika jenzi zake, tofauti na ilivyo sasa ambapo wamedai
TANROAD inafanya mambo yake pasipo kutaka ushauri wa wahandisi wenyeji.
Ernei Nyeho-
Diwani Kata ya Mdabulo amesema barabara nyingi zinazojengwa na TANROAD zimekuwa
chini ya kiwango kinachotakiwa, licha ya kuwa serikali imekuwa ikitoa fedha
nyingi tofauti naza Halmashauri, ambazo barabara zao licha ya kupatiwa kiwango
kidogo cha fedha, lakini zimekuwa ni imara na bora.
“Ukiangalia
barabara zetu za Halmashauri ambazo tunapatiwa fedha kidogo katika kuzijenga na
znuri sana tofauti kabisa na hizi za TANROAD, sasa mwenyekiti tunakuomba
utufikishie ujumbe kuwa hao TANROAD tunawataka wanapokuja Wilayani kujenga
barabara wawahusishe wataalamu wetu wahandisi wa Halmashauri, hii itasaidia
kupewa ushauri kwa maana ya vifusi,” Alisema Nyeho.
Tasil Mgoda
– diwani Kata ya saohill amesema ipo haja kwa serikali kuwa imara kuhakikisha
TANROAD inatengeneza barabara kwa kiwango kinachotakiwa, huku akitolea mfano wa
barabara ya Kinyanambo kwenda Kibengu kuwa imechakaa na haina hadhi ya kuwa
imetengenezwa na TANROAD.
Edna Mwikola- Diwani V/maalumu tarafa ya Ifwagi,
amesema hata alama za “X” zilizowekwa katika nyumba za watu kwa zaidi ya
miaka 3 hazionyeshi dalili zozote za
ujenzi wa barabara kuanza, licha ya
uwekaji wa alama hizo za “X” kwenye
nyumba za wananchi kusababisha madhara
makubwa.
“Baadhi ya
wananchi wamepoteza maisha, wamekufa baada ya nyumba zao kuwekewa alama za “X”,
hii inaumiza sana kwani barabara hizo mpaka leo hazina dalili zozote za
kujengwa, tunaiomba serikali itemize ahadi zake za kuzijenga barabara hizo
ambazo zimewekewa “X” kwani mpango huo umeleta madhara makubwa kwa
jamii”, Alesema Mwikola.
Naye mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Wilaya ya Mufindi Peter Tweve amesema ushirikishwaji wa masuala ya ujenzi wa miundombinu ya barabara utasaidia kutatua changamoto iliyopo, kwani wataalamu kutoka TANROAD wakati mwingine wamekuwa wakitumia Maram na vifusi visivyofaa kutokana na kutokuwa na wataalamu wenyeji.
"Hapa kinachotakiwa ni uwepo wa ushirikishwaji na ushirikiano, hii itasaidia kupunguza na hata kumaliza tatizo hili, mfano kuna wakati unakuta wataalamu wa TANROAD wanatumia Maramu na vifusi ambavyo haviendani na udongo wa eneo wanalotengeneza barabara, lakini kama wakiwashirikisha wataalamu wetu wa halmashauri wataepukana na hali hiyo," Alisema Tweve.
Meneja wa TANROAD
mkoa wa Iringa Injinia Paul Ryakurwa, akizungumzia mpango wa uwekaji wa alama za
“X” amesema hatua hiyo inasaisia kuwatahadharisha wananchi wasifanye maendelezo
yoyote katika hifadhi za barabara na kuwa mpango wa ujenzi wa barabara hizo upo lakini umekwamishwa
na uhaba wa fedha.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni