Mratibu wa Oparation Christimas Child- OCC mkoa wa Iringa- Mchungaji Boaz
Sollo wa kanisa la Overcomers la mjini Iringa, mara baada ya kukabidhi zawadi za watoto kwa wasimamizi wa vituo mbalimbali vinavyojihusisha na malezi ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu na hatarishi.
Baadhi ya walezi na wasimamizi wa vituo, wakiwa na
maboksi yenye zawadi mbalimbali za watoto kutoka nchini Marekani,
ambazo zimekabidhiwa na mratibu wa OCC mkoa wa Iringa- Mchungaji Boaz
Sollo wa kanisa la Overcomers la mjini Iringa.
Baadhi ya walezi na wasimamizi wa vituo, wakiwa na maboksi yenye zawadi mbalimbali za watoto kutoka nchini Marekani, ambazo zimekabidhiwa na mratibu wa OCC mkoa wa Iringa- Mchungaji Boaz Sollo wa kanisa la Overcomers la mjini Iringa.
Baadhi ya zawadi zinazotakiwa kuwafikia watoto, kila boksi moja ndani lina aina tatu ya zawadi, za elimu, afya na vitu mbalimbali vikiwemo vya michezo.
Mchungaji Sandagila wa Kanisa la KKKT Iringa, akihesabu vitabu kwa ajili ya kuviweka katika maboksi, ili kuwafikia kwa uhakika watoto wahitaji.
Jackson Konzo mratibu wa kituo cha PHM kituo cha watoto chenye watoto 105, waishio katika mazingira hatarishi, magumu na yatima cha Mwembetogwa mjini Iringa.
Said Ng'amilo akishuhudia zoezi hilo, kama mmoja wa wapiga picha maarufu wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa.
Baadhi ya viongozi wa vituo vya kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu, wakiendelea na zoezi la kuhakiki zawadi za watoto hao.
Mmoja wa viongozi wa vituo vya kulelea watoto akiwa amebeba Boksi kwa ajili ya kusafirisha kuwafikishia watoto hao walengwa.
Baadhi ya walezi na wasimamizi wa vituo vya kulelea watoto, wakiendelea na shughuli ya kuratibu zawadi, katika moja ya ofisi za kanisa la anglikani, yalipohifadhiwa maboksi hayo ya zawadi za watoto.
Zawadi za watoto njinsi zilivyo kwenye maboksi makubwa.
Wakijadili jambo, nje ya kanisa la Anglikan mjini Iringa, mara baada ya kupatiwa zawadi za watoto katika vituo vyao.
<<<HABARI>>>
KANISA la Overcomers
Power Center (OPC) la mjini Iringa limeingilia kati tatizo la watoto yatima,
washio katika mazingira hatarishi na magumu kwa kutoa misaada na zawadi za
kujikimu kwa watoto elfu saba wa mkoa wa Iringa.
Akikabidhi zawadi hizo kwa wasimamizi wa
vituo vya kulelea watoto hao, katika uwanja wa
kanisa la Anglikani la mjini Iringa, mratibu wa Oparation Christimas Child (OCC) mkoa wa Iringa Mchungaji Boaz
Sollo amesema msaada huo ni huduma ya
kimataifa kutoka nchini Marekani, chini ya mfuko wa msamaria “SAMARITAN’S PURSE”.
Mchungaji Sollo amesema mpango huo ni sawa na huduma
ya msalaba mwekundu (Red cross) nchini, kwa kuwa umekuwa ukijihusisha na ugawaji
wa misaada kwenye majanga mbalimbali, huku nchini Tanzania likiwagusa kundi la
watoto wadogo kuanzia miaka 2 na nusu hadi miaka 14-hususani yatima na waishio
katika mazingira magumu na hatarishi.
Aidha Sollo amesema jumla ya makontena kumi yameingia
nchini, ambapo msaada huo ukiilenga mikoa ya Pwani, Dare s salaam, Mwanza,
Kilimanjaro, Tanga, Mbeya, Morogoro, mkoa wa Iringa nk.
“Zawadi hizi zinatolewa na shirika la kimataifa la
Marekani, linalojihusisha na majanga, na lipo kama Redcross, kwani
linajihusisha na utoaji wa misaada mbalimbali kwa wahanga wa majanga mbalimbali,
na hapa nchini huduma hii ina zaidi ya miaka kumi na mpango huu ni kuonyesha upendo wa Mungu kwa watoto,” alisema.
….Katika kila boksi moja analopatiwa mtoto kuna zawadi
zinazolenga sekta tatu, ..sekta ya afya, elimu na michezo, na dhumuni kuu la
zawadi hizo likiwa ni kudumisha upendo kwa kundi hilo la watoto.
Amesema katika zawadi na misaada hiyo, mkoa wa Iringa umewahusisha
watoto wa Wilaya ya Kilolo, Iringa vijijini na Manispaa ya Iringa huku lengo ni
kuwafikia watoto wa Wilaya zote, ili kufikisha ujumbe wa huduma hiyo ya OCC.
Amesema mkoa wa Iringa umepatiwa kontena moja lenye box
elfu 7, lenye thamani ya shilingi Milioni 300, zawadi zitakazowafikia watoto zaidi ya elfu
saba, huku boksi moja likiwa thamani ya
shilingi elfu 50.
Amesema Samaritan’s Purse inatoa misaada na zawadi kwa
kundi hilo la watoto, kama ni moja ya janga, na hiyo ni kutokana na Tanzania asilimia
kubwa ya watoto kuwa katika mazingira magumu
na hatarishi.
Sayuni Haran ni mratibu mtendaji wa kituo cha
Compassio, cha kanisa la Anglikan la Ipogolo mjini Iringa, amesema kituo chake
kina zaidi ya watoto 2800, na kuwa msaada huo utasaidia kupunguza tatizo
linalowakumba watoto hao.
Sayuni amesema tatizo kubwa linalotokana na uwepo wa
kundi la watoto waishio katika mazingira magumu na hatarishi ni wazazi na
walezi kutowajibika ipasavyo katika suala zima la malezi.
Aidha amesema changamoto nyingine inayowakabiri watoto,
mpaka wakakimbilia mitaani, ni sababu ya vifo vya wazazi, kwani asilimia kubwa
watoto hao hawana wazazi wote wawili, huku wengine wakiwa ni Yatima wasio na baba
wala mama, jambo linalowakosesha huduma muhimu nazaza msingi na hivyo kuwa na
maisha magumu na hatarishi.
Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Iringa Josephine
Mwaipopo amesema msaada huo ni funzo kwa wananchi, na chamsingi jamii pasipo
kutegemewa misaada kutoka nchi nyingine, ili kuwafanya watoto hao wajithamini.
Hata hivyo Mwaipopo amewataka walezi na wasimamizi wa
vituo kuhakikisha misaada na zawadi hizo zinawafikia walengwa, ili kufikia
lengo lililokusudiwa, na kuwa ni aibu kwa mtu mzima kuchepusha zawadi hizo kwa
maslahi yake binafsi.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni