SERIKALI imesema
ipo mbioni kuanzisha sheria ya kuwadhibiti wafanyabiashara wote wakubwa
wanaokwepa kodi, ikiwa pamoja na kuwafutia misamaha yote ya kodi kwa, kwa madai kuwa kutowatoza kodi wafanyabiashara
hao kunachangia uchumi wan chi kudhorota .
Hayo
yamezungumzwa na Naibu waziri wa fedha Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia ni naibu
katibu mkuu wa Chama Cha mpainduzi CCM, wakati akizungumza na wananchi wa
Manispaa ya Iringa na wanachama wa CCM, katika uwanja wa Mwembetogwa mjini
Iringa.
Nchemba amesema
Taifa hili linajengwa na watumishi wa serikali pamoja na wafanyabiashara
wadogo, ambapo wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakikwepa kodi ikiwa pamoja na
kupewa misamaha isiyo na tija, jambo linalodumaza uchumi wa taifa.
“Ubaya sana
sikuzaliwa na chembe ya uwoga uwoga, nchi yetu inaendeshwa na kodi za
wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo wadogo, wale wakubwa wapo wanakwepa kodi
na wengine wanapata misamaha ya kodi hadi wanatucheka,” Alisema.
Amesema atapeleka
sheria itakayofuta misamaha ya kodi, na kuwa serikali inakosa fedha za
maendeleo kwa ajili ya utitiri wa misamaha, na kuwa kamwe hatakubaliana na utaratibu wa kuwanyonya wanyonge halafu
wale wenye uwezo wa kulipa kodi wakaendelea kukwepa.
Amesema atapeleka
sheria itakayofuta kwa kiwango kikubwa misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara wakubwa
wakubwa, kwa madai kuwa anahitaji kuona nchi ya Tanzania inakuwa kwa jinsi inavyotakiwa
kuwa, na kuwa atawaomba wabunge wamuunge
mkono juu ya suala hilo.
Pia amesema
hawezi kuendelea kuona walimu na askari ndiyo wanakuwa watu wa kubanwa kwa kukatwa mishahara yao ili kulipa kodi, na sasa ipo haja ya kuondoa misamaha.
Amewataka wananchi kupuuza mpango wa serikali 3 kwani ni mzigo mzito kwa serikali, na kuwa serikali hiyo ya tatu haitahusika
na suala lolote huku ikitumia zaidi ya Tirion nne, na kuwasihi wananchi waache
ushabiki wa siasa usio na maana.
“Hii serikali ya
tatu itachangia ongezeko la kodi kwenu, kutarudisha kodi ya mbwa, ya Paka,
Kichwa, Baiskeri na tutatoza hata mtu akiona zaidi ya mke mmoja, kwa hiyo ndugu
zangu wana Iringa tuache ushabiki, maana serikali hii ya tatu itahudumiwa na
nani,” Alisema Mwigulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni