Askari polisi "Feki" bandia akiwa ndani ya ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan Mungi.
Askari polisi bandia ambao wanadaiwa kutumia sare za jeshi la polisi kuwatapeli wananchi wakiwa katika ofisi ya polisi mkoa wa Iringa.
Askari polisi bandia ambao wanadaiwa kutumia sare za jeshi la polisi kuwatapeli wananchi wakiwa katika ofisi ya polisi mkoa wa Iringa.
Askari polisi bandia ambao wanadaiwa kutumia sare za jeshi la polisi kuwatapeli wananchi wakiwa katika ofisi ya polisi mkoa wa Iringa.
<<<HABARI>>>
ASKARI polisi feki wawili wanaotumia sare za Jeshi la Polisi nchini, wamekamatwa kwa kufanya utapeli, wakituhumiwa kutumia saere hizo kuwaraghai wananchi na kujipatia fedha.
Akizungumzia tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema askari hao bandia wametumia mbinu hiyo ya kuvaa nguo za Polisi kwa lengo la kujipatia fedha, huku
mmoja kati ya askari hao bandia akidaiwa kuwa na taaluma ya ualimu.
ACP Mungi amewataja askari bandia hao kuwa ni Rashid Nyakunga (20) mkazi wa Ilula Mtua, na mwezie akiwa ni Goodluck Mbeyale (21) mkazi wa Kihesa Iringa mjini, ambapo amesema utapeli huo wamefanya katika mikoa ya Iringa na Morogoro.
Aidha amesema vijana hao wote wamemaliza masomo yao katika shule ya sekondari Mtwivila ya mjini Iringa, na baada ya kumaliza kidato cha nne, mwinginbe alisomea ualimu na mwingine akiwa mfanyabiashara wa kurekodi muziki.
Akielezea namna walivyopata sare hizo Mungi amesema katika maelezo ya awali ya vijana hao - wamesema wamepatiwa na mmoja wa ndugu yao anayeishi mkoani Shinyanga ambaye ni askari Polisi.
Hata hivyo Mungi amesema kuwa sare hizo ziliibiwa katika moja ya mikoa hapa nchini na taarifa ya wizi huo iliripotiwa, na uchunguzi unaendelea ili kubaini zaidi juu ya wizi wa sare hizo.
Aidha Mungi amewataka wananchi kuwa makini na utaperi wa ajira, kwa madai kuwa jeshi la Polisi halitoi ajira kwa njia ya mitaani, la sivyo watatapeliwa na wajanja.
Amesema mafanikio hayo yametokana na mtego uliowekwa ambapo walifanikiwa kumnasa Askari bandia ambaye amekuwa akifanya utapeli huo kwa kutumia njia ya simu, huku akimshirikisha mtuhumiwa mwenzake aliyekuwa akitumika kama ni kiongozi mkubwa wa jeshi la Polisi.
Askari huyu feki
na mkuu wake wanadaiwa kutumia sale za jeshi la Polisi kujikusanyia fedha,
wakitoa ahadi kwa wananchi ya kuwapatia ajira katika jeshi hilo.
Hata hivyo wananchi wamelitaka jeshi hilo kujitafakari zaidi ili kutambua sare hizo zinakotoka, kwa madai kuwa zinaweza kuchangia kulichafua jeshi zima.
Wamesema kuna uwezekano baadhi ya askari wasio waaminifu ndiyo wanaosambaza sare hizo kwa raia, kwa lengo la kutumika kwenye uharifu mbalimbali.
Wamesema baadhi ya askari wasio na weredi wamekuwa wakijihusisha katika matukio mbalimbali ya kiharifu na hivyo kuharibu taswira nzima ya jeshi hilo na kupoteza imani kwa wananchi.
Mwaka 2013 polisi mkoa wa Iringa ilimkamata mwanamke raia wa Kenya, akiwa na sare za Watawa Masista wa Kanisa Katholiki ambapo Sista huyo alidaiwa kufanya utapeli katika mikoa mbalimbali hapa nchini na nchi jirani.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni