Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assah Mwambene
Mmoja wa wahadhiri wa chuo kikuu cha Iringa akizungumza na wahitimu wa kitivo cha habari katika siku ya habari chuoni hapo- ambapo mgeni rasimi alikuwa mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assa Mwambene.
<<<HABARI>>>
BAADA
ya kilio cha muda mrefu cha wanahabari juu ya sheria ya habari nchini, serikali
imeibuka na kusema tayari muswada huo upo tayari huku ikiahidi kuupeleka bungeni
ili kujadiliwa mara tu baada ya bunge la bajeti kumalizika.
Hayo
yameelezwa na mkurugenzi wa idara ya habari maelezo Assah Mwambene, wakati akizungumza
na wanafunzi wahitimu wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha Iringa, katika
maadhimisho ya siku ya habari chuoni hapo.
Mwambene
amesema muswada huo upo tayari na utapelekwa, na kuwa kikao chochote kinachohusika
na kutungwa kwa sheria muswada huo utajadiliwa,
Amesema
sambamba na sheria ya kusimamia vyombo vya habari, serikali imekamilisha utafiti
wa sheria ya haki ya kupata habari, ambapo imejifunza kutoka kwa nchi ambazo
tayari zina sheria kama hiyo ili kujidhatiti
na kupata sheria nzuri itakayofaa zaidi.
Mwambene
amesema katika sheria hiyo ya kusimamia vyombo vya habari kuna mapendekezo ya
kuwepo kwa bodi ya kusimamia taaluma ya habari ili kuwadhibiti watu ambao
hawana vigezo ambao wamekuwa wakiiharibu taaluma ya habari.
Amesema
katika sheria hiyo ambayo ndiyo itakuwa msingi pia wamependekeza kuwe na bodi itakayosimamia
taaluma ya uandishi wa habari ili kuweka vigezo vitakavyosimamia wanaofaa na
wasiofaa kuwa waandishi wa habari na wale watakaokosa vigezo kamwe
hawataruhusiwa kufanya kazi hiyo kama ilivyo sasa.
Mwambene
amesema lengo kuu la kuweka udhibiti na kuongeza heshima katika taaluma hiyo ili
ithaminiwe kama zilivyo taaluma nyingine, kwani watakuwa wamepunguza uwepo wa
wavamizi wa taaluma ya habari ambao wanafahamika kama “Makanjanja”.
“Katika
sheria hiyo ya uandishi wa habari ambayo ni msingi pia tumependekeza kuwe na bodi
ambayo itakayosimamia taaluma hii ya uandishi wa habari, bodi hiyo itasaidia kuweka vigezo vya msingi vitakavyosimamia
nani atakayefaa kuwa mwandishi hwa habari na wale watakaokosa vigezo kamwe hawataruhusiwa
kufanya kazi hiyo, hii bodi itaweka udhibiti pamoja na kuongeza heshima katika
taaluma hii ya habari ili ithaminiwe na jamii kama ilivyo kwa taaluma nyingine,
kwani bodi itapunguza uwepo wa “Makanjanja”, Alisema.
Aidha
Mwambene amewataka wanachuo hao wahitimu pindi waingiapo katika taaluma ya
habari kufanya kazi kwa weredi wa hali
ya juu, kwa madai kuwa jamii imekuwa ikiwategemea wanahabari katika kupata
masuala yenye uhakika kwa kuwa kada hiyo ina wajibu na umuhimu mkubwa katika
jamii.
Amewataka
kuwa makini na kutofanya kazi kwa ushabiki pasipo kucheza na taaluma yao ili
kuondoa changamoto zitokanazo na baadhi ya wanataaluma kutofanya kazi zao kwa
kufuata maadili ambayo ni miiko ya kazi yao.
Tumaini
Msowoya na Solomoni Lekui wanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu cha Iringa
ambao ni wasomi wa tasnia ya habari wamesema Muswada huo ni muhimu na umekuja
katika wakati muafaka, kwani utasaidia kupunguza changamoto zinazowakabiri
wanahabari, ikiwa pamoja na changamoto inayotokana na sheria ya mwaka 1976
inayotoa mamlaka makubwa kwa waziri husika kukifungia chombop cha habari wakati
wowote.
Nao
Wahadhiri wa chuo kikuu cha Iringa kitivo cha habari - Simon Berege na Rachel Yusuph
wamesema muswada huo ni mkombozi wa wanahabari, kwani hicho kimekuwa ni kilio
cha muda mrefu cha waandishi na kuwa sasa itasaidia wanahabari kufanya kazi kwa
ufanishi, ikiwa pamoja na kujenga demokrasia ya kweli nchini.
“Muswada
huo ukipitishwa na kuwa sheria utakuwa ni ukombozi kwa tasnia yetu, kwani
itaitengenezea heshima kwa kuweka viwango vya elimu na pia itasaidia kuwasukuma
wanahabari kwenda kusoma ili kukidhi vigezo vya kuwa wanahabari wanaotambulika,”
Hata
hivyo wameitaka serikali kuongeza muda wa kipimo cha uandishi kwa madai kuwa
muda wa miaka 63 ni mfupi na badala yake waongeze na kufikia miaka sita ili kutoa nafasi kwa wanahabari
kujiandaa na kujipanga kusoma na kufikia kiwango cha elimu ya shahada na
Stashahada (Diploma na Degree).
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni