Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - a.k.a "Mwarobaini" jina alilopewa na wananchi wa Pawaga baada ya kutatua changamoto zilizokuwa zikiwakabiri kwa muda mrefu.
Diwani wa Kata ya Itunundu Halfan Lulimi (Mwenye shati la Kijani) akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa, katika mkutano wa hadhara wa wakulima na wananchi wa Itunundu Pawaga.
Kulia ni mwenyekiti wa umoja "Tuungane" wa wakulima wa zao la Mpunga katika Kata ya Itunundu Pawaga- Wilaya ya Iringa akiwa na Twarib Abdlahaman Ubwa ambaye ni katibu wa Tuungane- wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika
mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na
katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
Mzee Mussa Kibuga (Mwenye Shati la Blue) akisikiliza kwa makini masuala yanayojadiliwa katika mkutano baina ya wananchi, wakulima, viongozi wa CCM na wale wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuhusiana na changamoto zinazowakabiri.
Baadhi ya wananchi wa Pawaga.
Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa
makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano
uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka.
MWAROBAINI.
Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga -Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika
mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na
katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
Baadhi ya wakulima wa zao la Mpunga -Pawaga wakisikiliza jambo kwa makini katika
mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano uliohudhuriwa na
katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka. MWAROBAINI.
Kulia ni mwenyekiti wa umoja "Tuungane" wa wakulima wa
zao la Mpunga katika Kata ya Itunundu Pawaga- Wilaya ya Iringa akiwa na
Twarib Abdlahaman Ubwa ambaye ni katibu wa Tuungane- wakiwa katika
mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wa Pawaga wakisikiliza jambo kwa
makini katika mkutano wa kujadili changamoto zinazowakabiri, mkutano
uliohudhuriwa na katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga - aka.
MWAROBAINI.
<<<HABARI>>>.
CHAMA cha
Mapinduzi CCM mkoa wa Iringa kimemaliza mgogolo + malalamiko baina ya wakulima wa zao la Mpunga na Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa, yaliyotokana na ongezeko la tozo la ushuru.
Wakulima hao wa
zao la Mpunga wa kata ya Itunundu na kata nyingine za Tarafa ya Pawaga wanaojihusisha
na shughuli za kilimo cha Mpunga wamekuwa wakilalamikia ongezeko la tozo la ushuru
kwa muda mrefu ushuru wa kutoka shilingi elfu moja hadi kufikia elfu mbili.
Wakifikisha
malalakimo yao kwa katibu wa CCM aliyefika katika tarafa hiyo kusikiliza kilio
cha wakulima hao, ambao wengi wao wapo chini ya Mwamvuli wa kikundi cha Tuungane,
katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kimande- baina ya
wakulima na viongozi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Iringa.
Twarib Abdulhaman
Ubwa katibu wa kikundi cha Tuungane cha wakulima wa zao la Mpunga amesema kupandishwa
kwa tozo la ushuru kumewafanya wanunuzi wa Mpunga kushindwa kuingia katika
tarafa yao kwa kwenda katika maeneo mengine ambayo hayana kiwango hicho cha
ushuru.
Ubwa amesema
hali hiyo ni pigo kubwa kwao kwani sasa wamekosa wateja hali inayowafanya wauze
Mpunga wao kwa bei ndogo kwa weanunuzi wachache wanaotokea, hali ambayo itawakwamisha
kuendesha shughuli hiyo.
“Kama unavyoona
kila nyumba ukipita ni magunia ya Mpunga, hayana wateja, hali hiyo imechangiwa
sana na ongezeko la Ushuru, wanunuzi wote ambao huwa tunawategemea hawafuiki
kwetu kununua Mpunga, wanakwenda katika maeneo mengine, hili ni janga na adhabu
hii wenye kuumia ni sisi wakulima sio wafanyabiashara,” Alisema Ubwa.
Ubwa alisema
kuna haja ya Halmashauri kupunguza tozo hilo na kufikia kiwango kile kile cha
awali, kwani changamoto hiyo ya ushuru kwa mtazamo wa kina unaweza kuathiri
masuala mbalimbali likiwemo la wakulima kushindwa kujikimu na hata kukwama
kulipa adha za watoto wao kwa kukosa fedha.
Naye Festo Elioti
Kulanga ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha Tuungane amesema gharama hiyo ya
ushuru wa shilingi elfu mbili kwa gunia moja, itawafanya wakulima kushindwa
kununua pembejeo na zana za kilimo za za kisasa.
Kulanga alisema
baadhi ya wenye magari nao wamegoma kupeleka magari yao kuchukua mpunga katika
eneo hilo kwa kuhofia ushuru mkubwa wa magari kwani gari moja limekuwa
likitozwa hata zaidi ya shilingi Milioni moja jambo ambalo halina tija kwa
mkulima, mfanyabiashara na hata msafirishaji.
“Katibu hapa
kero yetu kubwa sisi ni ushuru, kero ambayo tumeilalamikoa kwa muda mrefu licha
ya kupewa majibu kuwa wataitatua lakini hakuna kinachofanyika, ushuru ni mkubwa
sana, lakini pia wakala anayetoza ushuru amekuwa pia akijihusisha na rushwa
ambapo kila gari limekuwa likilipishwa shilingi milioni moja ,” Alisema.
Aidha alisema
kuna gari ya Maprosoo T. 910 AMV ambayo ililipishwa shilingi Milioni kwa gunia 120 alizopakia, ambayo
ni sawa na zaidi ya shilingi elfu 8 mia 8 na elfu 3 333 ilikuwa inaendeshwa na Feisary.
“Ilipita gari ya mtu anaitwa Medy gari namba T.600 AJV ililipa shilingi laki 642, 000
ambayo ukigawa kwa gunia moja ni sawa na shilingi 5352, na ilipita gari ya
Massey ambayo ililipa shilingi milioni moja sawa na shilingi 8333, na wenye
magari hao wamegoma kusafirisha mazao yetu mpaka tupate hitimisho la Ushuru huo”,
Alisema Kulanga.
Hata hivyo katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan
Mtenga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, amepiga marufuku utozaji wa
ushuru kwa mkulima anayesafirisha Gunia 1 hadi 6 za mazao, kwenda mjini au
Sokoni, kwa madai kuwa kuwabana kwa ushuru huo wakulima kutakwamisha kupata
fedha za kuendeshea shughuli hizo.
Mtenga ameiagiza
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kupitia mwenyekiti wake Steven Mhapa kuacha
mara moja tabia ya kuwatoza wakulima kiwango hicho cha ushuru, na kuwa watafute
namna nyingine ya kuongeza mapato ya Halmashauri pasipo kuwakandamiza wakulima,
kwa madai kuwa gharama hizo za utozwaji wa ushuru zinafifisha kaulimbiu ya
Kilimo kwanza.
Mtenga amesema
tatizo la baadhi ya viongozi kutokuitisha mikutano ya hadhara, linasababisha
malalamiko mengi kwa jamii, na hivyo baadhi ya wananchi kukimbilia vyama
pinzani, kwa kukosa sehemu ya kupata ufumbuzi wa changamoto zinazowakabiri.
Na kuwa viongozi
wote wanaokwepa majukumu ya kuwahudumia wananchi, atahakikisha anawachukulia
hatua kali za kinidhamu, kwa madai kuwa viongozi wa aina hiyo ndiyo wanaokwamisha jitihada za Chama cha
mapinduzi katika kuwaletewa maendeleo wananchi.
Hata hivyo
mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema ongezeko la
ushuru huo umelenga kutatua changamoto mbalimbali za wakulima, kwa kuboresha
huduma, huku akisema baadhi ya wakulima wamekuwa hawataki kubadilika pindi
wanapogeuka kuwa wafanyabiashara na malalamiko hayo ni njia ya kukwepa kodi.
Hata hivyo
uchunguzi uliofanywa umebaini ukubwa wa tatizo hilo, kwani kila nyumba katika
Tarafa hiyo yamejazana magunia ya Mpunga ambayo hayana wateja, jambo ambalo
linaweza likawakatisha tamaa ya kuendelea na shughuli za kilimo wakulima hao.
Kwa kawaida
msimu huu wa mwezi 6 Mpunga huuzwa kwa zaidi ya shilingi elfu 50 hadi 70 lakini
kutokana na hali hiyo wakulima hao wanalazimika kuuza shilingi 35 gunia lenye
debe 7 huku baadhi yao wakiwa wamekata tamaa kabisa hata kuvuna na hivyo
kuuacha Mpunga huo bado kwenye Majaruba ambayo yanamaji jambo ambalo ni hatari
katika sekta hiyo ya kilimo.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni