Moja ya eneo la shamba la miti la msitu wa Sao hill.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa - Jesca Msambatavangu, akizungumzia suala hilo la Vibali.
Katibu wa CCM - Wilaya ya Mufindi- Miraji Mtaturu, akiwa katika kikao hicho cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Iringa.
Ally Simba mmoja wa wajumbe wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Iringa akisikiliza jambo.
Katibu msaidizi wa CCM Mkoa wa Iringa - Jimson Mhagama akiwa katika kikao hicho ambacho kimetoa maazimio juu ya Vibali vya shamba la miti la Taifa- la msitu wa Saohill.
Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi - Miraj Mtaturu- ndani ya kikao hicho.
<<<HABARI>>>
WAZIRI wa
maliasili na utalii Razalo Nyalandu– ametakiwa kufuta vibari vyote vilivyotolewa katika msimu huu, vya
shamba la miti la Taifa la Sao hill, lililopo Wilayani Mufindi mkoani Iringa, kwa
madai kuwa utaratibu wa utoaji wa vibari uliotumika niwa rushwa na uliojaa
ufisadi, kwani hata watu waliokufa
wameorodheshwa kupewa fulsa hiyo.
Kauli hiyo
imetolewa na Chama cha mapinduzi CCM, kupitia mkutano mkuu wa Halmashauri ya
mkoa wa Iringa, ambapo wajumbe wa
mkutano huo wamemtaka waziri huyo wa
wizara husika ya maliasili na utalii kuchukua hatua hiyo ya kuvifuta vibari
hivyo, haraka ili kuwatendea haki wananchi wa Mufindi na mkoa wa Iringa.
"Ndugu wanahabari, tulikuwa na kikao cha kawaida cha kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabiri wananchi, tumekutana na wajumbe wa Halmashauri kuu ya mkoa, na kero kubwa ilikuwa niya Vibali katika shamba la miti la taifa la Saohill, vibali ambavyo havikutolewa katika utaratibu unaotakiwa," Alisema Msambatavangu
Jesca
Msambatavangu ambaye ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa akiwakilisha ujumbe wa
mkutano huo mbele ya vyombo vya habari, ametoa tamko hilo, na kumtaka mkuu wa
mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma kufikisha ujumbe huo kwa Waziri haraka
iwezekanavyo, ili kupunguza ujanza unaotaraji kufanyika.
Aidha
Msambatavangu ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wameonekana majina yao katika
orodha ya mgao wa vibali, huku wengine majina yao yakijirudia zaidi ya mara 20
(Ishirini) jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa msitu huo, kwakuwa asilimia
kubwa ya kundi la vijana na wenyeji wa mkoa wa Iringa hawajapata fulsa ya
kupatiwa Vibari.
“Tumesikia kuwa
tayari kuna mbinu wanazifanya, eti waliotoa vibari wamewaambia waliopatiwa
vibari hivyo walipie TRA mapema kama ni njia ya kuzuia kufutwa, tuwaambie tu
wananchi kuwa wasikubari kuingizwa katika hasara hiyo, kwani hata wakisajiliwa
hawawezi kupewa vibali watakuwa wameingia hasara bure,” alisema Msambatavangu.
Pia alihoji
kujiamini kwa baadhi ya viongozi hao wa msitu wa sao hill wanaojihusisha na
utaperi huo wa mali ya serikali, kwa madai kuwa wanalindwa na nani ambaye
nawapa ujasiri wa kufanya ubadhirifu huo mara kwa mara pasipoi kuwa na shaka na
woga wowote.
“Nasikia kuna
wananchi waliambiwa watoe shilingi Milioni 3 kwa kila kibali ili kuwa na
uhakika wa kupata nafasi hiyo ya kupata vibali, na watu hao waliolipa Milioni 3
kwa kila kibali, hela ambazo alikuwa anapokea mama mmoja na jina tunalo, tumepata
taarifa kuwa wamepata wote, kweli hili ni jambo la aibu sana kwa kiongoai wa
serikali kufanya ufisadi wa aina hii,” Alisema.
Katika safu ya
meza kuu walimtaka mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Ishengoma kuangalia vyema safu ya
uongozi wa bodi ya shamba – huku wakiitaka bodi hiyo wawepo wawakirishi wa
wananchi kama madiwani na wabunge ili wapate nafasi ya kuwatetea wananchi wao,
tofauti na bodi hiyo ilivyo sasa.
Pia
Msambatavangu amehoji uwepo wa viongozi wa Wilaya hiyo ya Mufindi- kwa madai
kuwa asilimia kubwa wanalifumbia macho tatizo hilo ambalo linawakosesha imani
wananchi dhidi ya serikali yao, hasa
wananchi wa Wilaya ya Mufindi ambao ndiyo wazimaji wakubwa wa moto pindi
unapoibuka katika shamba hilo la miti.
Pia amesema
mfumo wa uongozi wa shamba husika la
Saohill ndiyo una matatizo na kuwa viongozi wote wa serikali watakaobainika
kuhusika katika tuhuma hiyo watachukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuondolewa
katika nyadhfa walizonazo kwa madai kuwa hawawatendei haki wananchi.
Mapendekezo…wametaka
katika vibari 800 vinavyotolewa katika msitu huo, angalau vijana wapewe fulsa
ya vibali 300, ili kupunguza ukali wa changamoto ya ajira kwa kundi hilo, na asilimia
50 wanufaika wawe niwakazi wa mkoa wa Iringa na asilimia nyingine inayobaki iwe
nikwa manufaa ya watanzania wote, kwani msitu huo ni mali ya Taifa ila wakazi
wa Iringa wapewe kipaumbele zaidi.
Shamba la miti
la Taifa saohill, limekuwa likikabiliwa na changamoto ya ugawaji wa vibari –
kwa kupata tuhuma za kutoa fulsa hata kwa marehemu, huku baadhi ya wanufaika wakiwa ni viongozi, jambo ambalo mwaka 2012
liliilazimu Waziri mstaafu wa maliasili na utalii Barozi Hamis Kagasheki kuvifuta vibari 500 ambavyo
vilionekana ni mamluki.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni