SAKATA la
kampuni ya Green Miles Safaris Ltd, kufutiwa vibali vya uwindaji
nchini, limeibuka upya baada ya waziri kivuli wa maliasili na utalii mchungaji
Peter Msigwa kusema kamwe hakubaliani na hatua zilizochukuliwa na waziri Lazaro
Nyalandu.
Kauli
hiyo imetolewa na mchungaji Msigwa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iringa
mjini – kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, katika
mkutano wake wa hadhara, baina yake na wananchi wa Kata ya Mivinjeni Manispaa
ya mji wa Iringa.
Mchungaji
Msigwa amesema bado kuna hatua za muhimu zinazopaswa kuchukuliwa na Wizara hiyo
ya maliasili na utalii, ikiwa pamoja na kuwawajibisha watumishi wote ambao
hawakuwajibika ipasavyo, kwa kuruhusu kampuni hiyo kuvunja taratibu na sheria
za uwindaji.
Akitaja
watumishi wa idara hiyo wanaopaswa kuwajibishwa, Mchungaji Msigwa amesema
mtaalamu wa uwindaji “Professional Hunter”
ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kuchukluliwa hatua kwa kushindwa kuzuia
kampuni hiyo kuendelea na shughuli zake baada ya kukiuka sheria za uwindaji.
“Katika
masuala yale ya uwindaji waziri amechukua baadhi ya hatua yu, lakini kuna
madai mengine hajayafanyia kazi, mimi kama waziri kivuli
nilimuagiza afanye, kwanza nilisema watendaji wote ambao wamehusika kwa kutosimamia uwindaji kisheria
walipaswa wachukuliwe hatua lakini sijaona wamechukuliwa hatua kazi zaao
ipasavyo ilipaswa wasimamishwe, lakini sijamuona waziri amechukua hatua yoyote.
…Lakini
katika masuala ya uwindaji kuna mtu anaitwa “Profeshno hanta” ambaye yeye kama uwindaji unakiukwa kwenye vitalu
anatakiwa awasimamishe, na kama wanagoma kusimama anatakiwa atoe ripoti wizarani, kwamba hawa wawindaji
walikiuka sheria, kwa mfano hiyo kampuni ya
Green Miles Safaris Ltd walikuwa wanaua wanyama wa kike, walikuwa wanawaua
wanyama wadogo, lakini kulikuwa na muwindaji mwenye umri wa miaka 16, jambo
ambalo kiuwindaji haliruhusiwi, kwa hiyo waziri bado hajafanya mambo hayo,”
alisema Mchungaji Msigwa.
Pia
amesema wale wote waliohusika kwa kutosimamia ipasavyo sheria ya uwindaji - nao
wanapaswa kuchukuliwa hatua ikiwa pamoja na kuwajibishwa kwa kutokuwajibika na
siyo kuiwajibisha kampuni ya uwindaji pekee.
Hata
hivyo Msigwa amepongeza hatua ya waziri wa malisili na utalii- Lazaro Nyalandu kwa
kuvunja idara ya uwindaji , na badala yake kuweka mamlaka – ambapo amemtaka pia
waziri Nyalandu kuvifanyia uchunguzi wa
kina vibali vyote vya uwindaji ili kuokoa wanyamapori hao ambao ni rasilimali
kuu ya Taifa.
Alisema
endapo hatawawajibisha watendaji wa idara hiyo ya uwindaji, kikombe
walichokinywa mawaziri wa idara hiyo waliopita, kamwe Nyalandu naye
hakitamuepuka, kwa madai kuwa waziri huyo naye atapaswa kuwajibishwa au
kuwajibika mwenyewe.
Kufutwa kwa leseni za uwindaji kwa kampuni hiyo
kulitajwa na waziri Nyalandu kuwa kunatokana na
ukiukwaji wa sheria ya mwaka 2009 ya uwindaji wanyamapori – ambapo kwa
kupitia sheria hiyo kifungu namba 5 kinampa mamlaka Waziri mwenye dhamana
kufuta vitalu vya uwindaji kwa kampuni yoyote inayokiuka taratibu zilizowekwa.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni