Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa Wilaya bora nyanda za kusini.
Diwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Ritha Mlagala akizungumza jambo mara baada hya kupokea Kombe la ushindi wa kuwa
Wilaya bora nyanda za kusini. Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa.
Diwani wa Kata ya Izazi Wilaya ya Iringa akifurahia kupata ushindi huo wa Halmashauri yake kuwa bora kwa mkpoa wa Iringa na Halmashauri zlote za mikoa ya Kanda ya kusini.
Madiwani wakifurahia ushindi huo.
Diwani Shakira Kiwanga wa Kata ya Kalenga akifurahia kupata ushindi huo.
<<<HABARI>>>
HALMASHAURI ya
Wilaya ya Iringa imefanikiwa kuwa Wilaya bora, kati ya Wilaya za mikoa ya
kusini kwa shughuli mbalimbali za kilimo, ujasiliamali na ufugaji.
Sifa ya Wilaya
hiyo imetolewa katika maonyesho ya 22 ya sherehe za wakulima nanenane, ambazo
kanda ya kusini hufanyika katika uwanja wa John Mwakangale jijini Mbeya.
Mbele ya
viongozi, watumishi na wananchi mbalimbali wakiwemo wakulima, Wilaya ya Iringa imepewa
kombe la ushindi wa kwanza Kimkoa na kikanda kwa kuwa na sifa bora na
zinazokidhi vigezo katika mpangilio wa kazi zake za kilimo.
Akitanabaisha
namna Halmashauri yake ilivyofanikiwa kushika nafasi hiyo ya kwanza, mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema siri kuu ni ushirikiano
baina ya wao madiwani, watumishi wa halkmashauri yake pamoja na wananchi kwa
ujumla.
Aidha Mhapa
amesema pia walijipanga vyema katika kuonyesha shughuli halisi ziunazofanywa
katika Halmashauri yake, kikiwemo kilimo, ufugaji na masuala ya utalii ambayo
ni kielelezo cha mkoa wa UIringa ambo ni kitovu cha utalii mikoa ya nyanda za
juu kusini.
Akitoa wito-
Mhapa ameutaka uongozi wa uwanja huo kuhakikisha unaboresha miundombinu ya barabara,
kwa kuweka Lami katika barabara zake zote zilizopo katika uwanja huo.
Mhapa amesema changamoto
kubwa zilizopo katika uwanja huo, hazivumiliki, hasa uhaba mkubwa wa vyoo ambavyo haviendana
na takwimu ya wananchi wanaoingia katika uwanja huo.
“Uwanja huu
unakabiliwa na changamoto mbalimbali, mfano hali hii ya vumbi ni hatari sana,
tunataka barabara zote za ndani ya uwanja huu ziwekwe lami, lakini suala la
vyoo nalo ni tatizo kubwa sana, mfano hapa tulipo kwenye eneo la hii la jukwaa
kuna choo kimoja tu, hii ni hatari sana,” alisema Mhapa.
Naye Ritha Mlagala mmoja wa
madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, amesema kukosekana kwa huduma ya
vyoo vya kutosha katika uwanja huo, ni ni adha kwa wananchi wanaoingia katika
uwanja huo wa nanenane.
Maonyesho ya
nanenane yamefungwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabiti Mwambungu, akiwemo Abbas Kandolo mkuu wa mkoa
wa Mbeya, na maonyesho hayo kitaifa yamefanyika katika viwanja vya viwanja vya
Ngongo mkoani Lindi, na kufungwa rasmi
na makamu wa rais Mohamed Bilal.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni