Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha cha Iringa wakiwa nje ya jengo la chuo chao, mara baada ya chuo hicho kuzindiliwa rasmi na mamlaka ya vyuo vya ufundi stadi Tanzania - VETA.
Mwenyekiti wa bodi ya VETA Kabaka Ndenda- wa pili kushoto mara baada ya kuzindua chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa, akiwa na baadhi ya viongozi wa VETA mkoa wa Iringa, wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha Yohanes Nicorous Sanga.
Mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha
Yohanes Nicorous Sanga, akizungumza jambo mara baada ya chuo chake kuzinduliwa rasmi.
Kabaka Ndenda- mara baada ya kuzindua
chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa, akisikiliza jambo kwa umakini, kutoka kwa mkurugenzi wa Chuo cha utalii Ruaha
Yohanes Sanga (pichani hayupo).Mmoja wa viongozi wakuu wa VETA nyanda za kusini, akiwa katika siku ya uzinduzi wa chuo cha Utalii Ruaha- kilichopo Iringa.
Suzan Magani kaimu mkurugenzi wa VETA kanda ya nyanda za kusini, akiwa katika siku ya
uzinduzi wa chuo cha utalii Ruaha.
Bango la uzinduzi Bango la uzinduzi wa jengo la kulala wanafunzi- wa chuo cha utalii Ruaha.
Jengo la chuo cha Utalii cha Ruaha- Iringa. Chuo cha utalii cha Ruaha, kikiwa tayari kimezinduliwa rasmi.
Chuo cha utalii Ruaha- Iringa.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha wakiwa nje ya jengo lao.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha wakifurahia jambo baada ya chuo chao kuzinduliwa rasmi.
Baadhi ya Wanafunzi wa chuo cha utalii Ruaha Iringa wakiwa nje ya kati ya jengo la chuo chao.
<<<HABARI>>>
MAMLAKA ya vyuo
vya ufundi Stadi VETA imesema itahakikisha inavifungia vyuo vyote vinavyokiuka sheria
na taratibu, kwa kutokuwa na sifa ya utoaji wa elimu hiyo, kwa madai kuwa vinachangia
wahitimu wake kukosa fulsa ya ajira.
Kauli hiyo
imetolewa na mwenyekiti wa bodi ya vyuo vya Ufundi stadi VETA Kabaka Ndenda
wakati akizindua chuo cha Utalii cha Ruaha kilichopo Kalenga Wilaya ya Iringa,
chuo ambacho kitasaidia katika utoaji wa elimu ya sekta ya utalii na kuutangaza
mkoa wa Iringa.
Ndenda amesema mpango
huo umelenga kuokoa muda wanaopoteza wanafunzi kusoma katika vyuo hivyo visivyo
na sifa, kwa madai kuwa vinapoteza fedha za wazazi / walezi wa wanafunzi, jambo
ambalo linachangia ongezeko la vijana wasio na ajira.
Aidha ndenda
amesema katika kukabiliana na hali hiyo pia watawadhibiti wamiliki wa Hotel,
Motel na “Lodge” nyumba za kulala wageni ambao wanatoa ajira kwa wafanyakazi
wasio na elimu ya huduma ya hotel.
Ndenda amesema
waajiri wengi wamekuwa wakikimbilia kuajiri wafanyakazi wasio na sifa, ili
kulipa mishahara duni isiyoendana na viwango vinavyotakiwa na serikali, na kuwa
hata hivyo waajiri hao wanajimaliza wenyewe kwa kuwakabidhi kazi watu wasio na
taaluma.
Naye mkurugenzi
wa chuo cha utalii cha Ruaha -Yohanes Sanga amesema mpango huo utasaidia jamii
kuwa na elimu bora, kwa kuwa sasa kuna ushindani usio na tija, ambapo baadhi ya
walezi na wazzi wasio na uelewa juu ya usajili wa vyuo hujikuta wakiwapeleka
watoto wao katika vyo hivyo na hivyo kupata hasara ya fedha na muda.
Sanga amesema
kuna umuhimu jamii ikazingatia masuala ya elimu bora ya utalii, na kuachana na
kasumba ya kukimbilia unafuu wa ada, kwa kuwa jambo hilo ndilo linalowafanya
wahitimu kukosa ajira, baada ya vyuo vyao kutotambulika kisheria.
Sanga amesema
kumekuwa na ushindani mkubwa wa uendeshaji wa vyuo, hasa hivyo visivyo na sifa,
na kuitaka jamii kuwa makini kwa kufanya uchunguzi ili kutambua mapema- mapungufu
ya vyuo kabla ya kujiunga navyo.
“Ningeiomba
jamii isikimbilie unafuu wa ada, kuna vitu vya msingi vya kuzingatia hasa
usajili, utoaji wa elimu bora, lakini pia hata mazingira nayo yanatakiwa kuwa
mazuri na yenye muonekano unaovutia kwa wanafunzi -yawe rafiki kwa utoaji na
upokeaji wa elimu,” Alisema Sanga.
Sanga amesema kuanzishwa
kwa chuo hicho cha Utalii Ruaha ni mwarobaini wa kuinua hali ya utalii mikoa ya
nyanda za juu kusini, na hasa mkoa wa Iringa ambao umepewa dhamana ya kuwa kitovu
cha utalii mikoa ya kusini.
Aisha Sharif mwanafunzi
wa chuo cha utalii Ruaha amesema changamoto kubwa inayowakabili pindi
wanapojiunga na vyuo visivyo na sifa ni kupoteza muda wao walioutumia kusoma,
na pia kupoteza fedha za wazazi wao.
Naye Radhia
Abdullah ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho cha utalii Ruaha amitaka
serikali kuvifungia haraka iwezekanavyo vyuo vyote visivyokidhi sifa na vigezo
vya kutoa elimu, kwa kuwa vinaifanya taaluma hiyo ya Hoteli na utawala kutothaminiwa
katika jamii.
Mwanafunzi Furahini
Msigwa, ameiomba serikali kuvisajiri haraka vyuo vyote vinavyokuwa na sifa, ili
kutoa fulsa ya wanafunzi wengi kipata elimu hiyo, kwa kuwa baadhi ya vijana wamekuwa
wakipoteza dira ya maisha yao kwa kukosa nafasi ya kujiunga na vyuo hivyo vya
ufundi.
Wanafunzi hao wamesema kukamilika kwa chuo hicho, ikiwa pamoja na kuwa na vigezo ni majibu tosha kwa kundi lao vijana ambao kilio chao kikubwa ni juu ya upatikanaji wa ajira, kwa madai kuwa sasa watapata elimu ya utalii na hivyo kuwawezesha kupata ajira na kuondokana na utegemezi.
Kwa mujibu wa
mwenyekiti huyo wa bodi ya VETA -mikoa ya kusini ina jumla ya vyuo vya ufundi stadi
69 pekee, huku vinavyomilikiwa na mamlaka ya ufundi stadi yaani VETA vikiwa ni vyuo vitatu tu, 66
vikiwa nivya watu binafsi na taasisi mbalimbali.
Hata hivyo hali
hiyo ya ndiyo inayotoa mwanya wa uvunjaji wa sheria na kusababisha baadhi ya
wanafunzi kuangukia katika vyuo visivyosajiliwa na hivyo kujikuta wakikosa
ajira- kwa kuwa vyuo vyao havitambuliki.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni