Louis van
Gaal aliamua kumrudisha Rooney kutoka katika nafasi yake ya mshambuliaji
wa kati kumpeleka kuwa kiungo katika wiki za hivi karibuni, lengo lake
kubwa likiwa ni kuwapa nafasi Robin van Persie na Radamel Falcao kucheza
mbele yake.
Kucheza kama kiungo wa kulia siku ya
jumapili Rooney, ambaye ameshindwa kupiga shuti hata moja lenye malengo
kwa mwaka 2015, alishindwa kushika mpira katika eneo la boksi la
wapinzani wao West Ham- hii ni hali ya ajabu kwa mchezaji ambaye aliweza
kupachika mabao 10 katika michezo 9 iliyopita katika uwanja wa Upton
Park.
Lakini Muholanzi Van Gaal anaamini kuwa
kufanya hivyo kuna muwezesha yeye kutumia mfumo wake wa 4-3-1-2 ambao
anaamini kuwa Rooney anafurahia kwa sababu atakuwa anaenana na mfumo
wake.
“Sisemi kwamba kila siku atacheza kiungo
hapana hii inategemeana na mfumo wa siku hiyo upoje na aina gani ya
washambuliaji ninaotaka kuwatumia lakini katika mchezo unaofuata
nitamtumia kiungo mwingine." alisema Van Gaal
“Nafikiri anapenda kucheza nafasi ya kiungo kwa sababu muda wote anatafuta mpira,lakini anauwezo wa kucheza nafasi nyingi tu."
Rooney hajafanikiwa kucheza vizuri akiwa nafasi ya kiungo.
RECORDI YA MAN UTD NA BURNLEY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni