Jumatatu, 16 Februari 2015

UTATA WAENDELEA KUJITOKEZA NANI ATAKUWA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJI

  fredrick mwakalebela akizungumza na waandishi wa habari
 mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.
 fredrick mwakalebela akiwa na rais wa jamhuri ya muungano ya tanzania.

na mwanahabari wetu fredy mgunda,iringa.
 

wananchi na wananchama wa chama cha mapinduzi (ccm)wa manispaa ya iringa wameendelea na  sitofaham na ni mtu sahihi wa kugombea jimbo la iringa mjini kutokana na wagombea wengi kujitokeza katika harakati hizo.

wakizun gumza kwa nyakati tofauti wananchi na wanachama hao wamesemakuwa kuna watu ambao tayari wamejijengea majini katika harakati hizo ambao na jesca msambatvangu,fredrick mwakalebela na mahamood madenge wote wanasadikika kuingia kwenye kinyang’anyilo hicho.

ila mwanahabari frank kibiki, aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec ameonekana kuvurunga kabisa plani za wanachama kutokana na kuoneka ni kiongozi anayefaa kuigwa na kila lika inayomzunguka.

wakizunguza kwa nyakati tofauti wanachama wa chama cha mapinduzi wamesema kuwa frank kibiki ndiye mtu pekee anayeweza kureta upinzani kwa mbunge wa jimbo hili mchungaji peter msigwa kutokana na kujiamini kwake.

wameongeza kwa kusema kuwa  frank kibiki anaushawishi mkubwa kwa jamii tofauti na na watu wengine wanaopanga kugombea jimbo hilo kwa sababu anasiasa safi na sera ambazo zinatekelezeka  kulingana na mazingara ya wananchi wa manispaa ya iringa.


pia waliongeza kuwa wananchi wanahamu ya kumfahamu frank kibiki kutokana na jina lake kukua kwa ghafla na kuwaguza wanachi wengi hivyo inapelekea siku hadi siku kumtafuta na kutaka kumjua yeye ni nani na anafanya nini.

walimalizia kwa kusema kuwa kibiki ni mtu pekee ambaye anaweza kuwaweka wanachama cha mapinduzi pamoja kutokana na kutokuwa na kundi hata moja ndani ya chama tofauti na wagombea wanaotarajiwa kugombea jimbo hili.

kwa upande wake katibu wa ccm mkoani iringa hassani mtenga alisema ipo siku kwenye kura za maoni watu watazimia hii ni kutokana na baadhi ya watu nwanaotarajia kugombea jimbo hili wamekuwa wakitumia pesa nyingi kuwaonga wananchi ili wamchague na akasisitiza kuwa uongozi sio pesa uongozi ni kipaji na uwezo wa mtu binafsi aliopewa na mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni