KAIMU MENEJA WA SIDO MKOA WA IRINGA, MR NIKO MAHINYA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFINI KWAKE
KAIMU MENEJA WA SIDO MKOANI IRINGA, NIKO MAHINYA AKIWA NA MHANDISI WA
KARAKANA YA SIDO IRINGA, MICHAEL MATONYA WAKATI WAKITEMBELEA UTENDAJI
KAZI WA KARAKANA HIYO
FUNDI WA KARAKANA YA SIDO ELAYSON TARIMO AKIANGALIA MASHINE YA KUNOA VYUMA, AMBAYO ILIKUWA IKINOA MAJEMBE YA KUKATIA CHAI
MSIMAMIZI WA KARAKANA YA KUTENGENEZEA MASHINE MBALIMBALI YA SIDO MKOANI
IRINGA, LEONARD LUMATO AKIENDELEA NA KAZI KATIKA KARAKANA HIYO
KIJANA AKIENDELEA NA KAZI NDANI YA KARAKANA
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO), mkoani Iringa limewataka
watanzania kujenga utamaduni wa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani, badala
ya zile zinazoingizwa kutoka nje ili kukuza uchumi wan chi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa, Kaimu meneja
wa SIDO mkoani Iringa, Niko Mahinya alisema ikiwa watanzania wataenzi bidhaa
zinazotengenezwa ndani itakuwa rahisi kuinua uchumi wa nchi, na mtu mmoja
mmoja.
Alisema shirika hilo limekuwa likitengeneza bidhaa nyingi,
zikiwemo mashine na pembejeo za kilimo lakini, kutokana na dhana ya kununua
bidhaa za nje wamekuwa wakikabiliana na tatizo kubwa la soko.
“Tunazalisha mashine mbalimbali, zikiwemo zana za kilimo kama
vile, mashine za kusagia nafaka, kuchujia mafuta ya alizeti, kukamulia asali na
nyingine nyingi lakini changamoto kubwa ni soko la bidhaa za ndani,”alisema
Aidha alisema itakuwa vyema kama serikali itaweka utaratibu
au sera itakayofanya watu wajenge tabia ya kuheshimu, kupenda na kutumia bidhaa za ndani.
Kwa upande wao baadhi ya wajasiriamali na wakulima walisema
kuwa mara nyingi wamekuwa wakinunua mashine za kichina kutokana na bei yake kuwa
chini ingawa hazina ubora.
“Bidhaa za nje ni bei ndogo kuliko zile zinazotengenezwa
ndani, hii ndiyo sababu inayofanya wengi tutumie bidhaa za kichina ambazo hata
hivyo hazidumu kwa muda mrefu,”alisema LeoniKA Sanga, mmilikiwa kiwanda cha
kukamua mafuta ya alizeti, mjini Iringa.
Aliiomba serikali kutoa ruzuku kwa SIDO ili bidhaa
zinazotengenezwa zishushwe bei yake na kuweza kuwahudumia wajasiriamali na
wakulima wadogo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni