DJ
Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya
kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa
wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni
ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na
vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za kuingiza pesa,
kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao pamoja na
kuwaburudisha.
"Nimeamua
kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na
kuweka mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu
zinakaribia kuwa kweli".
Story
ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia
kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti la
Mwanaspoti, kuanzia JUMAMOSI HII ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho,
utapata ideas mbali mbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na
kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo,
Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.
DJ Tee akiwa studio.
Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee
ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za
redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo
kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!
Wewe
pia USIKOSE kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa
kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii
(28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye
ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina @djtee255
Studio.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni