Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina mabula- akisisitiza jambo katika moja ya mikutano yake.
<<<HABARI>>>
VIONGOZI wa
serikali za mitaa- vijiji na vitongoji, wametakiwa kuwasaka kwa udi na uvumba
wanafunzi wote ambao mpaka sasa hawajajiunga na
masomo ya elimu ya Sekondari, huku viongozi hao wakiagizwa kuwachukulia
hatua za kisheria wazazi ambao wataonekana
ni sababu ya watoto wao kutoanza elimu hiyo ya sekondari.
Tamko hilo
limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula, mara baada ya kupatiwa
taarifa ya tatizo la utoro wa wanafunzi wa shule ya sekondari Mkwawa, iliyopo
katika Manispaa ya Iringa, ambapo zaidi ya wanafunzi 40 mpaka sasa hawajaripoti
kuanza masomo.
Mabula amesema ili
kukabiliana na hali hiyo- watendaji wanapaswa kutambua idadi ya wanafunzi ambao
mpaka sasa hawajaripoti shuleni, na taratibu za kuwafuatilia majumbani zianze mara moja- ili kufahamu
sababu za watoto hao kutoungana na wenzao kuanza kidato cha kwanza.
Evod Luwanda -
mkuu wa shule ya Sekondari Mkwawa amesema jumla ya wanafunzi 120 pekee ndiyo wameshajiunga
na elimu ya sekondari, na wanafunzi 40 hawajafika mpaka sasa- huku kati yao 16 akiwa
hana taarifa zao, wakati wanafunzi 24 wakiwa wamejiunga na shule binafsi kwa ridhaa ya wazazi na walezi wao.
“Mh. Mkuu wa
Wilaya.. mpaka sasa ni wanafunzi 120 ambao wamesharipoti na wanafunzi 24
wamekwenda kusoma shule nyingine kwa ridhaa ya wazazi na walezi wao, huku wengine
31 wazazi wao wakijipanga kuwaleta shuleni, na hiyo ni kulingana na hali ngumu ya
uchumi,” Alisema Luwanda.
“Mh. Mkuu wa
wilaya tatizo la utoro linatusumbua sana shuleni hapa, mfano katika matokeo ya
mwaka jana 2014, waliofeli ni wale wanafunzi 7 watoro lakini mwaka huu tumedhamilia
kukabiliana na hali hiyo kwa kuhakikisha utoro tunaupunguza kama siyo kuufuta
kabisa,” Alisema Mwalimu Luwanda.
Aidha Mwalimu
Luwanda amesema changamoto nyingine inayowasumbua ni pamoja na shule kukosa Maabara,
na kutokuwepo ushirikiano wa kutosha baina ya baadhi ya wazazi na walimu, hasa
katika suala la michango.
Amesema ili
kuendesha shughuli za shule zinazohitaji fedha, hulazimika kukopa fedha kwa
wadau ambao ili kufanikisha masuala ya kitaaluma, na kuwa wadau huisaidia sana shule,
na hiyo ndiyo sababu inayosababisha shule kuwa na madeni makubwa.
Kunibert Kivinge
afisa mtendaji wa Kata ya Mkwawa- amesema watatumia njia ya mgambo kuwakamata
wazazai wa wanafunzi ambao mpaka sasa hawajafika shule kwa madai kuwa idadi ya
watoto hao inafahamika na kitakachofanyika ni kutafuta majina ya wazazi tu.
Hata hivyo wanafunzi hao ambao mpaka sasa hawajaanza masomo tayari wamepoteza siku 90 tangu shule za sekondari kote nchini zifunguliwe- January
2015.
Kuyakosa masomo kwa muda huo, mpaka sasa tayari wamepoteza
vipindi 420, kwa wastani wa masomo 7 kila siku, na idadi hiyo nikwa
mahudhurio ya siku tano ndani ya wiki moja – kuanzia juma tatu hadi ijumaa kwa kipindi cha miezi hiyo mitatu.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni