Jumamosi, 4 Januari 2014

"FAWE na TUSEME" MARUFUKU WATOTO KUTUMIKISHWA KATIKA AJIRA


 Baadhi ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, kambi iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ. Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Bi. Neema Kitundu- mratibu wa FAWE Taifa akisikiliza maoni ya watoto katika kambi iliyowakutanisha watoto wa shule za msingi kutoka Wilaya sita, - Wilaya ya Makete, Mbeya Vijijini, Mtwara, Temeke, Mufindi pamoja na Iringa vijijini.
 Bi. Sophia Komba mmoja wa viongozi wa mradi wa FAWE akizungumza na jopo la watoto wa shule za msingi kutoka katika Wilaya sita nchini, katika kambi iliyofanyika katika shule ya sekondari JJ. Mungai Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
 Baadhi ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, wakionyesha ubunifu wao wa kuchora michoro inayoendana na mafunzo ya kupinga ukatili na unyanyasaji wa watoto, ambao unachangia baadhi yao kuikosa elimu.
 Baadhi ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, kambi iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ. Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
 Baadhi ya watoto washiriki wa kongamano la kambi lililoandaliwa na shirika la FAWE kwa kushirikiana na UNICEF chini ya mradi wa TUSEME, kambi iliyowekwa katika shule ya sekondari JJ. Mungai katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
 Baadhi ya walimu ambao waliambatana na wanafunzi wao katika kambi hiyo wakisikiliza maoni ya wanafunzi hao juu ya ukatili wanaofanyiwa.
 Watoto kutoka Wilaya ya Temeke wakitoa ushuhuda kupitia maigizo kama ni sehemu ya ushiriki wao katika kambi hiyo.

 Watoto washiriki wa kambi la wanafunzi kutoka Wilaya sita nchini wakitoa ushuhuda juu ya vitendo vya ukatili vilivyopo katika jamii wanamoishi.

SHIRIKA la FAWE chini ya mradi wake wa TUSEME nchini Tanzania  limepiga marufuku mtindo wa baadhi ya wazazi na walezi kuwatumikisha watoto wenye umri wa kwenda shule, katika shughuli mbalimbali ambazo ni kikwazo katika elimu.

Hayo yamezungumzwa na mratibu wa FAWE nchini Bi. Neema Kitundu katika kongamano la watoto   wa shule za msingi kutoka Wilaya tisa nchini, ambapo amesema tatizo la watoto kutumikishwa bado lipo katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, pamoja na Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Bi. Kitundu amesema tatizo hilo halina tofauti na ukatili wa kijinsia, na kuwa hali hiyo imeshamiri sana katika Wilayani Mufindi ambapo watoto hutumikishwa kama vibarua katika mashamba ya Chai, huku wengine wakitumiwa katika ajira za kazi za nyumbani.

Aidha Bi. Kitundu amesema katika Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya nao wanaukatili kwa watoto hao wadogo, na kuwa wao huwatumia watoto katika mashamba ya Mpunga, jambo linalowafanya wakose kwenda shule.

“Tumeona bado kuna changamoto  kubwa kwa watoto hawa, na katika wilaya tunazozifanyia kazi tumetambua Wilaya ya Mufindi inawatumikisha watoto katika mashamba ya Chai, huku Wilaya ya Mbarali watoto wengi wanafanyishwa kazi katika mashamba ya Mpunga, jambo hili ndugu zangu linakwamisha sana sekta ya elimu, na halina tofauti na ukatili wa kijinsia, kwani watoto hawa wanaikosa fulsa muhimu ya elimu,” Alisema Kitundu.

Amesema baadhi ya watoto wamekuwa wakitoroka shule na hata kutokwenda kabisa na kukimbilia katika ajira hizo na hivyo kupoteza muda wa masomo, jambo ambalo linaashiria kukosekana kwa elimu kwa watoto hao na hivyo Taifa kuwa na watu wasio na elimu.

“Katika Wilaya ambazo tumezifikia tatizo la ajira za utotoni tumetambua bado zipo kwa Wilaya ya Mufindi na Mbarali, na wengi wetu hasa tunaotoka Dar es Salaam tumekuwa na dhana ya kuwa wasichana wa kazi za ndani wazuri wanatoka Mufindi Iringa, na kule Mbarali wao wanajihusisha sana na kilimo cha Mpunga, na wakati wa kilimo watoto wengi wanashinda mashambani, na hata wazazi wapo radhi kuomba ruhusa shuleni kwa kisingizio kuwa mtoto swake anaumwa kumbe anamfanyisha kazi za shambani, si wavulana si wasichana” Alisema

Amesema FAWE kwa kushirikiana na UNICEF walifanya kazi kwa wilaya kumi, na sasa wameanza na Wilaya sita ambazo ni Wilaya ya Makete, Mufindi, Njombe, Mbeya vijijini, Iringa Vijijini na Wilaya ya Mbarali.

Amesema mradi FAWE kwa kushirikiana na UNICEF umeweza kuleta mafanikio makubwa, kwa kupunguza tatizo la wanafunzi wa kike kuacha masomo kwa kupata mimba, ambapo  mwaka 20006 kabla mradi haujaanza kufanyakazi mimba zilikuwa zaidi ya 400 kila mwaka kwa shule za msingi pekee, na shule zilizokuwa ndani ya mradi wa FAWE mimba zilikuwa 166 kwa mwaka, na mafanikio yamepunguza tatizo hilo la mimba hadi ambapo mwaka 2013 mimba zimebaki tatu pekee.

Naye mwasisi wa FAWE nchini Profesa Penina Mrama amesema FAWE kwa kushirikiana na TUSEME inamsaidia mtoto kupata elimu ya utambuzi wa haki zake za msingi na kuondoa ubaguzi baina ya watoto wa kike nawa kiume.

Profesa Penina amesema kupitia mradi wa FAWE na TUSEME  wameweza kuwaokoa watoto wengi ambao walikuwa tayari wameikosa elimu, na sasa wamejikita zaidi kulielimusha kundi hilo kutambua haki zao ili waweze kuzitetea.

Na kuwa shirika limekuwa likitoa afua za kusaidia sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu wezeshi kama Maktaba, Maabara, Mabweni y Chakula, utoaji wa Vitabu nk. yote hayo yakiwa yamelenga kuyafanya mazingira ya elimu kuwa rafiki kwa wanafunzi ili kuvutia na kuipata elimu pasipo na vikwazo vovyote. 


Aidha Profesa Penina amesema pia mradi unapingana na vitendo vya ukatili vinavyochangia mtoto kushindwa kupata elimu, zikiwemo ajira pingamizi kwa sekta ya elimu.

Hata hivyo shirika la kazi duniani (ILO) katika ripoti yake iliyotolewa mjini Geneva kuna zaidi ya watoto milioni 10.5 duniani wanatumikishwa kazi za nyumbani katika  mazingira magumu.

Katika ripoti hiyo Shirika la Kazi Duniani ,limeeleza kwamba watoto hao wanafanya kazi za usafi, wanapika,wanatunza bustani na pia wanafanya kazi ya uyaya, hiyo ikiwa haina tofauti kabisa na ripoti ya FAWE katika Wilaya zake inazozifanyia kazi, ambako changamtoto hizo za kazi kwa watoto nazo zimejitokeza kwa kiwango kikubwa.

ILO ilienda mbali zaidi na kusema katika ripoti yake kuwa watoto milioni sita na nusu  wanaofanyishwa kazi za majumbani wana umri kati ya miaka 5 na 14  na zaidi ya asilimia 71 ni wasichana.

Pia ILO ilibainisha kuwa watoto wengi wanaoajiriwa majumbani mara nyingi hawalipwi ujira stahiki na waajiriwa wao, huku baadhi ya waajiri wakidiliki hata kuwabagua , jambo linalojenga dhana potofu katika vichwa vya Taifa hilo la kesho.


Na hali hiyo ya ajira kwa kundi la watoto isipopigiwa kelele inaweza kuongezeka zaidi kila mwaka kutokana na mahitaji  ya watumishi wa nyumbani, kutokana na ukweli kuwa asilimia kubwa ya wananchi wanajishughulisha na kazi mbalimbali na hivyo kuwa na uhitaji mkubwa wa wafanyakazi wa kazi za nyumbani.

Huenda hali hiyo ya ajira kwa kundi la watoto wadogo likaongezeka zaidi na zaidi kutokana na wanawake wengi kupata kazi nje ya nyumba  hali inayotofautiana na siku za awali ambapo mwanamke alionekana kuwa ndiye muhusika mkuu wa kazi za nyumbani za kuihudumia familia.


MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni