Wafuasi na wanachama wa CHADEMA wakisindikiza msafara wa mgombea wao kurudisha fomu ya ushiriki wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga.
Wafuasi wa CHADEMA
Bw. Godfrey W. Mgimwa mgombea wa CCM akirudisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la kalenga Bi. Pudensiana Kisaka.
Wafuasi na wanachama wa CCM wakimsindikiza mgombea wao kurudisha fomu ya kushiriki mchakato wa kampeni za kiti cha ubunge jimbo la Kalenga.
<<<<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>>>>
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA na Chama Cha Mapinduzi CCM leo wamefanikiwa kurudisha fomu za kushiriki
kugombea nafasi ya kiti cha Ubunge wqa jimbo la Kalenga mkoani Iringa, nafasi
iliyoachwa wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, Dk William Mgima ambaye pia
alikuwa Waziri wa fedha kupoteza maisha januari 1, mwaka huu nchini Afrika
Kusini wakati akipatiwa matibabu.
CHADEMA, CCM na CHAUSTA wamerudisha fomu hizo
leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kurejesha fomu, fomu ambazo zitawapa nafasi ya kugombea nafasi hiyo, huku wagombea wa vyama
vya NCCR-Mageuzi na Chausta wakiwa ndiyo wamechukua fomu hizo siku ii ya
mwisho.
CCM ambayo ilikuwa ya kwanza
kurudisha fomu za mgombea wake majira ya saa tano asubuhi na kufuatiwa na
Chadema waliorejesha fomu zao majira ya saa saba mchana, kupitia wagombea wao
Godfrey Mgimwa (CCM), Grace Tendega
(CHADEMA na Richard Minja wa CHAUSTA
Wagombea wa vyama vyote viwili
walisindikizwa na maandamano ya wafuasi na wanachama wao na kufanya shamrashamra
ziwavutie wananchi wengi mjini Iringa.
Akiwa na wafuasi zaidi ya 500,
mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa aliyetokea ofisi za CCM Iringa Vijijini zilizopo
mjini Iringa, alisindikizwa hadi kwa msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na baada ya domu zake kupokelewa
aliendelea na maandamano yaliyoishi ofisi kuu za CCM Mkoa wa Iringa.
Grace Tendega aliletwa katika ofisi
za msimamizi huyo wa Uchaguzi jimbo la Kalenga akiwa na msafara wa pikipiki 20 na
magari 5, huku mgombea wa CCM pamoja na wafuasi na wanachama wake wakitembea
kwa miguu hadi katika ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa.
Katika nasaha zao kwa wapiga kura wa
jimbo hilo, wagombea hao wamewataka wafuasi wao kufanya kampeni za amani na
kuepuka lugha au matendo yanayoweza kuhatarisha amani na ustaarabu.
Akizungumzia kauli ya Rais Jakaya
Kikwete ya hivikaribuni inayowataka wana CCM kuacha unyonge, Mgimwa alisema
haikuwa na maana kwamba wana CCM hawawezi kupambana na wapinzani wao.
“Kauli ile ilikuwa na maana
tuwafundishe wenzetu ustaarabu ili waache siasa za vurugu na machafuko,”
alisema.
Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya
Iringa, Delphina Mtavilalo alisema
hawawezi kutumia silaha kupambana na wapinzani wao, watatumia maneno kupambana
nao.
“Tulipata uhuru bila kumwaga damu;
tunatoa onyo kwa vijana wetu wakiona kuna mapambano yanayohatarisha maisha yao
watoe taarifa kwenye vyomo vya dola, kwa kufanya hivyo watakuwa wanaondoa
uonnyonge wao,” alisema.
Naye Mgombea wa Chadema, Tendega
aliwataka wafuasi wa chama hicho kuondokana na dhana waliyonayo ya baadhi ya
watu kuona kwamba wao ni watu wa fujo, na akiwataka sasa kufanya kampeni za kistaarabu.
“Nawaomba wana Kalenga na wana
Chadema kwa ujumla, tufanye kampeni za amani katika kuleta mabadiliko ya
kisiasa na kiuchumi nchini,” alisema.
Kampeni za uchaguzi huo mdogo
zitaanza kesho Februari 19 na kuhitimishwa Machi 15, ambapo tarehe 16 mwezi huo
wa tatu ndiyo utafanyika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo la kalenga.
Hata hivyo …majira ya saa kumi na
moja mtandao huu ulifanya mawasiliano na msimamizi wa uchaguzi Bi. Pudensiana
Kisaka kujua kama vyama vya NCCR na CHAUSTA kama vimefanikiwa kurejesha fomu
zao na majibu yalikuwa ni “Chama cha NCCR kimechelewa kurudidisha fomu na licha
ya hivyo bado baadhi ya masharti kilikuwa bado hakijakidhi, kwa hiyo
nimewaondoa kwenye ushiriki wa kugombea kiti cha Ubunge jimbo la kalenga na
CHAUSTA wao wamefanikiwa kukidhi vigezo, kwa hiyo vyama vitakavyoshiriki
uchaguzi huo mdogo ni CHADEMA, CCM na CHAUSTA”, alisema Pudensiana Kisaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni