Ijumaa, 14 Februari 2014

CCM WACHUKUA FOMU JIMBO LA KALENGA

 Geofrey Mgimwa mgombea Ubunge jimbo la Kalenga mkoani Iringa akisaini moja ya fomu.
  Geofrey Mgimwa mgombea Ubunge jimbo la Kalenga mkoani Iringa akisaini moja ya fomu.


 Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Bi. Amina Himbo (wa kwanza kulia) akisikiliza jambo katika ofisi ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa mara tu baada ya mgombea wa Ubunge Geofrey Mgimwa kuwasiri katika ofisi hiyo.

 Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kalenga Bi. Pudensiana Kisaka, ambaye pia ni mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Wilaya ya Iringa akimkabidhi Bw. Mgimwa katiba ya nchi, baada ya kusaini fomu mbalimbali za kushiriki ubunge jimbo la Kalenga.
Mgombea ubunge Bw. Geofrey Mgimwa akisikiliza jambo kabla ya kuchukua fomu ya kushiriki ubunge jimbo la Kalenga.
 Baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Iringa walioshiriki katika hafla hiyo kama ni sehemu ya mchango wao katika kumuunga mkono Bw. Mgimwa katika shughuli ya uchukuaji wa fomu ya ushiriki wa mchakato wa Ubunge.
 Bi. Shakira Kiwanga diwani Kata ya Kalenga, akiwa na Mwenyekiti CCM Wilaya ya Iringa Bi. Delphina Mtavilalo  (katikati) na mwisho ni Mwenyekiti CCM Mkoa wa Iringa madam Jesca Msambatavangu katika hafla hiyo.
 Bi. Shakira Kiwanga akisikiliza jambo katika hafla hiyo.

 Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga Bw. Geofrey Mgimwa akiwapungia mkono wanaCCM waliofika katika ukumbi wa "Siasa ni Kilimo" alikofika kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Kalenga.
 
 "Ndiyo nimekubali kufuata masharti kwa namna fomu hii itakavyonielekeza"  ni Geofrey Mgimwa akipokea fomu kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la kalenga.

  Mmoja wa wasimamisi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la kalenga Bw. Evans wangipolini akimuelekeza Bw. Mgimwa namna ya kuijaza fomu hiyo.
 Fomu ya kugombea ubunge, ilivyo kabla haijajazwa na Bw. Geofrey Mgimwa.
 

 Baadhi ya wadhamini wakiwa na mgombea huyo ndani ya osfisi ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa.
Baadhi ya wanahabari mkoani Iringa akiwemo mmiliki wa mtandao huu Oliver Motto wakimsubiri nje ya jengo la CCM Mkoa wa Iringa Bw. Geofrey Mgimwa kufanya mahojiano naye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni