Ijumaa, 21 Februari 2014

UOKOTAJI WA KUNI WANAFUNZI IDODI KUOKOLEWA NA BIOGASS


 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Idodi wakiwa wanaokota "kuzagaa" kuni za matumizi ya chakula shuleni hapo.
 Kuni za leo afadhari ni kavu kidogo, maana ingenyesha mvua hapa chamoto ningekiona, zinakuwa nzito kwa ubichi" Anawaza kimoyo moyo.
 Hii ni hatari, hasa kwa wadudu kama Nyoka, Ng'e na wanyama.
 "Sasa haya ndiyo masomo, adhabu au ndiyo maisha ya Boarding??" Kama anajiwazia mwenyewe.
 "Karibu tunafika jamani".


 "Duu!! tumefika shule, tupo hoii" ni kama wanawaza katika nafsi zao.
 Aaah!! "Afadhari mizigo tumeitua"- Kama wanawaza hivyo kimyakimya
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Haman Tanzania Limited, ya jijini Dar es salaam- Mashaka Kalamba- kampuni inayojenga mitambo ya Biogass.
  Mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayojenga mradi huo wa Biogass- kutoka kampuni ya Haman Tanzania Limited, ya jijini Dar es salaam- Mashaka Kalamba akifafanua jambo kuhusiana na mradi wa ujenzi wa Biogass.
Fundi akiendelea na kazi katika moja ya mitungi minne ya Biogass itakayookoa mateso ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi- Iringa.
Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa mtungi wa Biogass.






Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa mitungi ya gess.



HABARI
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Idodi iliyopo katika Wilaya ya Iringa wapo katika hatari kubwa ya kuuawa na wanyamapoli baada ya kulazimika kuokota kuni katika msitu uliopo jirani na hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kuni ambazo zinatumika shule kwa ajili ya mpango wa chakula.

Wanafunzi hao wanasema licha ya kupoteza muda wa masomo kwa kufanya kazi hiyo, lakini pia usalama wao upo mashakani, kwa sababu shughuli hiyo ya uokotaji wa kuni hufanyika katika Msitu uliopo jirani na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo hukutana na wanyama pamoja na wadudu kama nyoka, huku baadhi yao wakidhurika kwa kuumwa na wadudu hao.

Timotheo Mlamka mwanafunzi wa shule hiyo amesema pia kuna hofu ya wanafunzi wa kike kufanyiwa vitendo viovu ukiwemo ubakaji.

Jerphasia Chengula amesema kuna baadhi ya siku wamekuwa wakikumbana na matukio ya ukatili ikiwemo kupigwa na wananchi wa kabila la Kimasai ambao husema wanachukua kuni zao.
Yohanes Kunzugala amesema msimu wa mvua kama sasa wanapata shida jinsi ya kuzipata kuni, kwani miti mingi huwa mibichi.

Mkuu wa shule ya Sekondari Idodi Christopher Mwasomola anakiri kuwepo kwa shida hiyo ya wanafunzi kuokota kuni, na kusema hali hiyo itaisha siku si nyingi, kutokana na kuwa serikali kupitia wakala wa Nishati ya umeme vijijini– Rural Energy Agency (REA)  imeanza ujenzi wa mitungi ya umeme mbadala.

Mwasomola amesema  kukamilika kwa ujenzi wa mitambo hiyo kutawanusuru wanafunzi wake na adha zitokanazo na uokotaji wa kuni msituni.

Aidha Mwasomola amesema hofu kubwa ni juu ya msitu huo kuwa jirani na hifadhi ya Taifa ya Ruaha na hivyo kuwepo baadhi ya wanyama ambao ni tishio kwa wanafunzi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayojenga mradi huo wa Biogass- kutoka kampuni ya Haman Tanzania Limited, ya jijini Dar es salaam- Mashaka Kalamba ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha ujenzi wa biogass amesema REA imegharamia shilingi milioni 140 katika ujenzi huo ambao utawawezesha wanafunzi kupata mwanga na kuokoa matumizi ya kuni.

 Kalamba amesema amesema baada ya kukamilika wanafunzi wataepukana na adha hiyo ya uokotaji wa kuni kwa ajili ya kupikia chakula cha wanafunzi.

“Tunategemea kuukamirisha mradi huu mwezi wanne mwaka huu, mitambo hii imejengwa chini ya ardhi ambapo nishati yake itazalishwa na kinyesi cha wanafunzi wenyewe, ndiyo maana unaona mabomba haya yanaelekea vyooni, na huko tumejenga vyoo vya kisasa, lakini changamoto ambayo ipo ni hii hali ya hewa ya mvua, ambapo mvua ikinyesha maji yanajaa kwenye mashimo haya kwani bado tunaendelea na ujenzi, kwa hiyo  hutulazimu kutumia mitambo “Pump”ya kuvuta maji.

Amesema changamoto nyingine ndogo ni umbali wa upatikanaji wa vifaa, kwani hulazimika kutembea km 78 kutoka mjini kwenye maduka ya vifaa vya ujenzi hadi eneo la ujenzi Idodi.

“Tunajenga mtambo mkubwa wenye Qubic mita 200 ambapo katika mitungi minne - kila mtungi unakuwa na Qubic mita 50 na kila mtungi utatoa gesi ya Qubic mita 18 ambayo itatoshereza mahitaji ya kupikia chakula kwa siku,” Amesema.

Shule ya Sekondari Idodi mnamo mwaka 2009 ilikumbwa na janga kubwa la Kitaifa, ambapo wanafunzi 12 wa kike walifariki dunia kwa kuteketea kwa moto, baada ya bweni walilokuwa wamelala kutokea hitirafu.

MWISHO



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni