Jopo la wanahabari mkoani Iringa wakiwa katika viwanja vya Mahakama ya Rufaa mkoa wa Iringa, huku mwanahabari Frenk Leonard aliyevaa shati la draft na Suruali ya kaki, kabla ya kupatwa na mkasa huo.
<<<<HABARI>>>>>
KATIKA hali isiyo ya kawaida, mwandishi wa habari wa gazeti
la Habarileo, na mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Iringa Frank
Leonard amekamatwa na askari Polisi wanne waliokuwa wamevaa kiraia kwa madai ya kupiga
picha mahakamani.
Tukio hilo limetokea leo asubuhi wakati jopo la wanahabari
likiwa limefika mahakamani hapo ili kufahamu mwenendo mzima wa kesi ya aliyekuwa
mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten marehemu Daud Mwangosi, ambapo mshtakiwa wa mauaji hayo alifikishwa katika mahakama hiyo.
Baada ya kukamatwa mwanahabari huyo Frenk, alifikishwa katika
kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa, na akizungumza na wanahabari baada ya
kuachiwa huru, Leonard amesema hali hiyo inaonyesha kuwa bado wapo baadhi ya
askari kwa makusudi wanataka kubomoa mahusiano yaliyopo baina ya wanahabari na
jeshi la Polisi ambayo yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Iringa, Ramadhani Mungi.
Aidha Leonard amesema
kitendo cha kubambikiziwa tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea
(mahakama) ni kitendo cha uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba
wanahabari ni watu wasiotaka kufuata taratibu za kimahakama, ambapo mwanahabari
huyo alikamatwa na askari akiwa ndani ya chumba cha mahakama pasipo idhini ya
Jaji wa Mahakama Kuu.
Msajili wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan
Nduguru amesema ameshangazwa na Polisi kwa kuingia shughuli za mahakama kwa
madai kumkamata mwandishi huyo kama alikuwa na kosa lilikuwa ni jukumu la
Mahakama na polisi walipaswa kupewa agizo na Jaji Mfawidhi aliyekuwa
anasikiliza kesi hiyo, ambapo Leonard ameachiwa huru katika kituo hicho baada
ya kukosekana kwa ushahidi wa kile kilichodaiwa kuwa mwanahabari huyo alivunja
taratibu na sheria za kimahakama.
Baada ya kukamatwa Leonard,
alifikishwa kituo cha Polisi cha Kati mjini Iringa na kuachiwa huru baada ya
kukosekana ushahidi,na akizungumza na wanahabari baada ya
kuachiwa huru, Leonard alisema "wapo baadhi ya askari kwa makusudi
wanataka kubomoa mahusiano baina ya wanahabari na jeshi la Polisi ambayo
yanaendelea kujengwa na kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani
Mungi."
Alisema kitendo cha kubambikiziwa
tuhuma ndani ya muhimili wa dola unaojitegemea (mahakama) ni kitendo cha
uzalilishaji kinachotaka kuaminisha umma kwamba wanahabari ni watu wasiotaka
kufuata taratibu za kimahakama.
Alisema akiwa ndani ya chumba cha
mahakama hiyo alikamatwa na askari hao bila idhini ya Jaji wa Mahakama Kuu
wakati akizima simu yake ya mkononi iliyokuwa katika mtetemo.
"Nilikuwa nazima simu yangu hao
askari hao kwasababu wanazojua wao wenyewe waligeuza suala hilo ili lionekane
katika sura wanayoitaka na hatimaye wanifungulie mashtaka," alisema.
Alimshukuru Mkuu wa Upelelezi wa
Wilaya ya Iringa, Ngoi kwa kumtendea haki na baada ya kupata ushahidi kufutilia
mbali kesi hiyo.
Akizungumza na wanahabari, Msajili
wa Mahakama Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Dunstan Nduguru aliwashangaa Polisi
kwa kuingia shughuli za mahakama.
"Hata kama mwandishi huyo
angekuwa anapiga picha, haikuwa kazi yao kumkamata mpaka wapewe agizo na Jaji
Mfawidhi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo," alisema.
Pamoja na askari hao kuwazuia
wanahabari kuchukua picha mara baada ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani,
Nduguru alisema utaratibu wa mahakama unawaruhusu wanahabari kuchukua picha
kabla shughuli kabla shughuli za mahakama hazijaanza na baada ya shughuli hizo
kwisha.
"Kuwazuia wanahabari kufanya
kazi zao kwa utaratibu huo sio sahihi; siku nyingine mkiona kuna dalili ya
kupata bugudha kama hiyo naomba mnijulishe ili niondoe mzozo huo,"
alisema.
Mbele ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama
Kuu Tanzania Kanda ya Iringa, Mary Shangali, Wakili wa upande wa mashtka,
Adolph Maganga alisema Adolph Maganda alisema kwa kukusudia mtuhumiwa
Pacificius Cleophace Simoni anatuhumiwa kumuua Mwangosi kinyume na kifungu cha
sheria ya kanuni ya adhabu namba 196 sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka
2002.
Alisema katika tukio hilo
lililotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani
Iringa, mshtakiwa alifyatua bunduki yake na kusababisha kifo cha marehemu, papo
hapo.
Alisema siku ya tukio marehemu
alikuwa Nyororo kwa ajili ya kuripoti na kutoa taarifa kwa umma juu ya mkutano
uliokuwa ufanywe na katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Alisema mshtakiwa akiwa mmoja wa
wafanyakazi wa Polisi, waliwasihi Chadema wasifanye mkutano huo kabla wafuasi
wake hawajaanza kurusha mawe kwa Polisi na baadhi yao kupata majeraha.
Kutokana na mzozo huo, wakili huyo
wa serikali alisema polisi walipiga mabomu ya machozi ili kuwatawanya wafuasi
hao kabla mshtakiwa huyo hajamfyatulia bomu marehemu.
Wakili huyo aliwasilisha ramani ya
eneo la tukio, ripoti ya mtaalamu wa milipuko na ripoti ya daktari
aliyechunguza mwili wa marehemu Mwangosi na gazeti la Mwananchi la Septemba 3,
2012 lililochapisha picha ya tukio hilo katika ukurasa wa mbele kama
vielelezo vinavyohusiana na kesi hiyo.
Wakili wa upande wa utetezi Lwezaula
Kaijage alitaja mambo wanayokubaliana katika kesi hiyo kuwa ni jina na anuani
ya mshtakiwa na kwamba marehemu Mwangosi alikufa kifo ambacho si cha kawaida.
Na kwamba mshtakiwa Simoni
alikamatwa na amefikishwa mahakamani akihusishwa na mauaji hayo.
Wakili Kaijage alisema vielelezo
vingine vilivyoletwa na upande wa mashtaka hawakubaliani navyo kwakuwa
vinahitaji ushahidi kutoka kwa wahusika.
Jaji Shangali aliahirisha kesi hiyo
mpaka kikao kingine cha mahakama kuu kitakapoitwa ili ianze kusikilizwa.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni