Jumapili, 27 Aprili 2014

CCM - WARIOBA ASHTAKIWE NA ARUDISHE BIL. 68 ZA MCHAKATO WA KATIBA

Katibu wa Chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Mufindi- Miraj Mtaturu , akifafanua jambo kuhusiana na tume ya katiba, katika kijiji cha Kimilinzowo, kilichopo Kata ya Itandula Mufindi.
 Mjumbe wa kamati ya saisa Wilaya ya Mufindi na Iringa Godfrey Mosha akielezea changamoto za serikali tatu kwa wananchi wa kijiji cha Kiliminzowo.
 Marcellina Mkini - Mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa (NEC) na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi akifafanua jambo.
 Miraj Mtaturu katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi.


 <<<<HABARI>>>>

CHAMA cha mapinduzi CCM kimeitaka tume ya Taifa iliyokusanya maoni ya Katiba mpya kurejesha fedha zote zaidi ya shilingi Bilioni 60 ambazo walipatiwa kwa ajili ya kukusanya maoni.  

Hayo yamezungumzwa na katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa- Miraji Mtaturu katika mkutano wake na wananchi wa kijiji cha Kimilinzowo kilichopo Kata ya Itandula Wilayani Mufindi.

Mtaturu amesema kuna haja ya Mwenyekiti wa tume hiyo ya katiba,  Jaji mstaafu Joseph Warioba kushtakiwa kwa kufuja fedha za watanzania alizopatiwa, kwakuwa kazi aliyotumwa haijafanywa kwa usahihi.

Amesema takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu laki tatu na elfu hamsini na sita waliotoa maoni,  watu laki mbili maoni yao hayakuchambuliwa, huku watu laki moja na hamsini na moja pekee ndiyo waliyochambuliwa.

Aidha amesema maoni ya mabaraza ya katiba ya wilaya hayajaingizwa katika orodha ya watu waliotoa maoni na kutokana na hali hiyo jaji warioba atatakiwa kutoa maelezo juu ya shilingi Bilioni 68 zilizotolewa kwa lengo la kuendesha Tume ya ukusanyaji wa maoni, kwa kuwa amepindisha maoni ya watanzania.

Naye Godfrey Mosha mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya na mkoa wa Iringa amewataka wajumbe wa bunge la katiba kufanya kazi waliyotumwa, pasipo kutumia vibaya fedha ambazo ni kodi za wananchi.

Mosha amesema viongozi wa upinzani wanaoshawishi wananchi kuipigia kura serikali tatu huku wakibeza uwepo wa Muungano walipaswa kujiudhuru, kwa kuwa mambo wanayoyafanya kwa uhuru ni matunda tosha ya Muungano wa Tanganyika na zanzibar.

"Ninamshangaa sana Tundulisu na kwani ndoa yao waliyoifunga na kwenda zanzibar kuwashauri wananchi kuishabikia serikali tatu n atangu lini CUF na CHADEMA wanawa marafiki wakati hata ndoa hiyo hata ya mkeka haifai, lakini sisi wana CCM tutaendelea kufunga kwani wale ni watanizetu lakini hawana siasa za kistaarabu, kwani wanajua kabisa kuwa chama kitakachoendelea kutawala, kusimamia misingi iliyowekwa na mwalimu Nyerere ni CCM,??  

Aidha amesema CCM ni chama dume ambacho hakina ukabila wala udini, jambo linalosababisha uwepo wa amani, upendo na utulivu mpaka sasa, tofauti na vyama vingine ambavyo hata muundo wake niwa kiukabila na ukanda.

Hata hivyo amesema jimbo la Iringa ambalo wameliazima kwa chadema kupitia mbunge mchungaji Peter Msigwa, sasa wamejipanga vyema kulichukua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Marcellina  Mkini - ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (NEC) na mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Mufindi amesema wanawake wanapaswa kuwa na msimamo pasipo kuyumbishwa na mtu yoyote, kwa kuwa pindi machafuko yanapotokea wanawake na watoto ndiyo hupata shida zaidi, na hivyo hakuna haja ya kutangatanga kuchangua vyama vya siasa zaidi ya CCM chama chenye kudumisha amani na utulivu kwa wananchi wake.
MWISHO




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni