Jumamosi, 10 Mei 2014

WENGINE 31 WATIMKIA CCM



 Mwenyekiti wa CCM tawi la chuo kikuu cha Mkwawa- Thea Ntara, akizungumza na wajumbe katika kikao/ hafla ya baadhi ya wanachama wa CHADEMA kujiunga na CCM .
Katibu wa UWT Manispaa ya Iringa Chiku Mohamed akiwa katika kikao hicho katika ukumbi wa hakuna kulala uliopo Mkwawa Iringa mjini.
Christopher Ngubiagai (katikati) MNEC na katibu mkuu vyuo vya elimu ya juu CCM  akizungumza jambo katika hafla hiyo ya kuwapokea wanachama wapya.
 Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga akitoa usia kwa wanachama na wajumbe, katika hafla hiyo ya kuwapokea wanachama wafya waliojiunga na CCM.
 Diwani wa kata ya Mkwawa "Kikulacho" akizungumja jambo na wanachama wa CCM tawi la chuo kikuu cha elimu Mkwawa
 Wanachama wa CCM Tawi la chuo kikuu Mkwawa wakisikiliza jambo katika hafla ya kuwapokea wanachama wapya.
 John Komba mmoja wa viongozi wa CCM Iringa, akitoa usia kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.
 Wanachama wapya waliojiunga na Chama cha mapinduzi CCm Wakiapa imani ya chama hicho.

 Diwani wa Kata ya Mkwawa "Kikulacho" akifungua Shampeni kama ishara ya kuwapokea rasmi wanachama hao wapya.
 Wilson Mwakaluba aliyekuwa naibu katibu CHADEMA tawi la mkwawa akipeana mkono na viongozi wa CCM mara baada ya kutangaza rasmi kujiunga na CCM.
 Christopher Ngubiagai (wa kwanza kulia) ambaye ni MNEC na katibu mkuu vyuo vya elimu ya juu CCM akiwa na Daniel Muhanza- (Katikati) ambaye ni katibu UVCCM Wilaya ya Iringa na wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa CCM tawi la Mkwawa Thea Ntara,wakifurahia jambo katika hafla hiyo ya kuwapokea wanachama wapya zaidi ya 30 waliojiunga na CCM.
Daniel Muhanza- (Katikati) katibu UVCCM Wilaya ya Iringa,akiwa na mwenyekiti wa CCM tawi la Mkwawa Thea Ntara, pamoja na   MNEC - Christopher Ngubiagai ambaye pia ni katibu Mkuu vyuo vya elimu ya juu CCM, (kwanza kulia).

 <<<<<<<<<<HABARI>>>>>>>>
HATIMAYE lile jinamizi la wanachama na wafuasi wa Chama cha demokrasia na maendeleo Chadema kukimbilia Chama cha Mapindizi CCM limeendelee baada ya wanachama 31 kujiunga na  CCM.

Wanachama hao ambao ni wafanyakazi na watumishi wa chuo kikuu cha elimu Mkwawa mkoani Iringa  tawi ambalo lina wanachama zaidi ya 320 wa CCM, wamejiunga na CCM kwa madai ya kuongeza nguvu ya utekelezaji wa irani ya CCM lengo likiwa ni ushindi katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Wakikabidhi kadi za CHADEMA kwa katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga katika tukio hilo lililofanyika Kata ya Mkwawa katika shule ya Chekechea ya hakuna kulala, wanachama hao wamesema maamuzi hayo yamelenga kulikomboa jimbo la Iringa mjini linaloshikiliwa kwa sasa na cHADEMA..


Akizungumzia hali hiyo, mwenyekiti wa tawi hilo, ambaye pia ni mkufunzi wa Chuo cha Mkwawa Thea Ntara amesema kati ya idadi ya wanachama hao zaidi ya 300,   wanachama 135 ni watumishi wa chuo hicho huku 171 wakiwa ni wanafunzi.

Ntara amesema wanachama na wanafunzi katika chuo hicho wanathamini sana masuala ya siasa ili kudumisha amani na utulivu na mahusiano mazuri kati ya watumishi na wanafunzi wenyewe, tofauti kabisa na siku za awali ambapo masuala ya siasa yaliibua hisia tofauti, fujo na hata makundi ya pande hizo mbili.

“Pale ndani ya chuo kuna wafanyakazi wenye imani mbalimbali za vyama, lakini kutokana na jinsi tunavyowafundisha, hakuna fujo wala migogolo tena kwani hata wakikutana wanazungumza na kupingana kwa hoja tofauti kabisa na hali ya zamani ilivyokuwa,” Alisema.

Aidha amesema hali ya utulivu na amani Mkwawa iliyopo imesaidia kuinua hata hali ya kielimu,  kati ya vyuo vitatu vinavyotoa mafunzo ya ualimu Mkwawa inaongoza ikifuatiwa na chuo kikuu Dar es salaam na kisha DUCE Chang’ombe.

Aidha amesema licha ya uwepo wa mafanikio hayo pia kuna changamoto, ikiwemo ya ukosefu wa ofisi ili kuendesha na kuratibu masuala yao ya kichama, licha ya kuwa ofisi ya Kata imekuwa ikiwasaidia kwa kuwaruhusu kufanya kazi zao katika ofisi hiyo ya Kata.

Amesema wamejipanga kukiimarisha chama kwa kutafuta mbinu za kuboresha uhai wa chama, kwa kutafuta mbinu mbadala za kukifanya chama hicho kiwe makini na imara zaidi ikiwa pamoja na kuisaidia jamii kwa kadri watakavyoweza.

“Katika kujijenga kichama chuo chetu kinasahauliwa sana katika michakato ya chama au kiserikali, toka ngazi za Wilaya, Mkoa na hata Taifa, mfano..Ni vijana wangapi toka Mkwawa wamepata ajira ndani ya CCM,  ni vijana wangapi wa Mkwawa wamepata fulsa ya kujifunza namna ya kuendesha kampeni za chaguzi mbalimbali ndani ya chama chao?? Hilo tunaomba lifanyiwe kazi, lakini pia chuo chetu ambacho nicha Serikali chenye jina kubwa Mkwawa.. hakijapata nafasi ya kutembelewa na viongozi wa serikali, jambo hilo linazua maswali mengi, tunaomba ujumbe huu ufike mapema kbla ya mwaka 2015,” Alisema Ntara.


Ntara amewataka wajumbe wa Katiba kuvumilia wakati wa kujadili masuala ya kuiandaa Katiba mpya, huku akiwasihi wakae pamoja ili kutekeleza adhma ya wananchi, kwa madai kuwa endapo Katiba haitapatikana kwa njia ya amani Watanzania hawana mahala pa kukimbilia.

Hatua hiyo ya CCM kuwakomba wanachama wa CHADEMA inakuja baada ya chama hicho kudhamiria kurudisha jimbo la Iringa mjini Mikononi mwao, jimbo ambalo lilichukuliwa na CHADEMA likiongozwa na mbunge Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Akijinasibu katika hafla hiyo, katibu wa CCM Mkoa wa Iringa Hassan Mtenga amesema hawana masihara juu ya mpango huo wa kuhakikisha jimbo la Iringa linashikiliwa na CCM na mikakati ni kutimiza ilani ya chama ili jamii ijenge imani na kisha kukiunga chama chake katika harakati za kuleta maendeleo.

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia warioba ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, aliwataka wanachama wa CCM kutoona aibu kukitangaza chama chao kwa kuvaa sare bila ofu, kwa madai kuwa baadhi ya wanachama wanaona aibu kuvaa nguo za chama hicho jambo ambalo linaonyesha kutokomaa kisiasa.


Dk. Warioba amewataka wanachama wa chama hicho kujivunia unachama wao kwa kuitangaza CCM kwa nguvu zao zote….“Mbona makada wa vyama vingine wanajivuna wanapovaa sare za vyama vyao,  utamaduni huo ni wa CCM lakini hali ni tofauti kidogo siku hizi, wanaCCM wengi wanaogopa kuvaa sare zao mbele ya watu wasiowajua,” alisema.

Hali ya pilikapilika na purukushani za kisiasa zinakuja ukiwa umebaki mwaka mmoja pekee, ili uchaguzi mkuu ufantike, wa kuwachagua Madiwani, wabunge na rais, uchaguzi utakaofanyika mwaka 2015, ambapo CCM imeanza kujiimarisha katika ngazi mbalimbali, ikiwa pamoja na katika taasisi za elimu ya juu mkoani Iringa ambako huko inasadikika kuwa kuna nguvu kubwa ya siasa.

MWISHO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni