Jumatano, 4 Juni 2014

TUME YA HAKI ZA BINADAMU KUWAANGUKIA WANANCHI

 Alfred Machumu- Mchunguzi mkuu wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, akiwa katika kikao cha utangulizi baina ya  viongozi wa Soko na  Tume ya haki za binadamu na utawala bora ndani ya ofisi ya Soko kuu la Iringa.
 Augustino Ngao makamu mwenyekiti wa Kikundi Cha Wafanyabiashara wa  "KBWS" akiwa katika kikao cha utangulizi cha viongozi wa Soko na viongozi wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora ndani ya ofisi ya Soko kuu la Iringa.
 Kushoto- ni Jafary Sewando- mjumbe wa KWBS Iringa, akiwa na Ezekia Chaula ambaye naye ni mjumbe, wakiwa katika kikao na watu wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora.
 Wilfred Warioba- Mchambuzi mkuu wa mfumo wa habari na mawasiliano wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, akiwa katika kikao hicho.

 Catherine Charwe mwanasheria wa Manispaa ya Iringa akiwa na Said Senjele kaimu mkuu wa Soko kuu wakiwa katika kikao na viongozi wa tume ya haki za binadamu na utawala bora.
 Mwanasheria wa Manispaa Catherine Charwe.
 Aldo kaduma katibu wa Soko kuu Iringa akiwa katika kikao na viongozi wa Tume.
 Aldo kaduma katibu wa Soko kuu Iringa akiwa katika kikao na viongozi wa Tume.
 Alexander Sales Hassan kaimu mkurugenzi wa elimu na mafunzo kwa umma kutoka Tume ya haki za binadamu na utawala bora, akizungumza na viongozi wa Soko Iringa.
 Alexander Sales Hassan kaimu mkurugenzi wa elimu na mafunzo kwa umma kutoka Tume ya haki za binadamu na utawala bora, akizungumza na viongozi wa Soko Iringa.
 Alexander Sales Hassan kaimu mkurugenzi wa elimu na mafunzo kwa umma kutoka Tume ya haki za binadamu na utawala bora, akizungumza na viongozi wa Soko Iringa.
  Kushoto ni Ezekia Chaula mjumbe wa soko- akiwa na Wilfred Warioba mchambuzi mkuu wa mifumo ya habari na mawasiliano kutoka tume ya haki za binadamu na utawala bora.
 Kushoto ni Beatrice Nkongo- mhasibu wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, wakiwa katika kikao cha utangulizi cha elimu ya ufikishaji wa malalamiko ya wananchi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi-"SMS".
 Kushoto- ni George Mwaitege mjumbe wa KWBS  akiwa na baadhi ya viongozi wa tume na soko hilo.
 Mwanasheria Catherine Charwe akiwa na kaimu mkuu wa Soko kuu Iringa, Said Senjele.
 Mwanasheria Catherine Charwe akiwa katika kikao hicho na viongozi wa tume.
 Mwanasheria Catherine Charwe akifafanua jambo katika kikao cha tume ya watu wa haki za binadamu na utawala bora, viongozi wa masoko Manispaa ya Iringa juu ya mfumo mpya wa uwasilishaji wa malalamiko ya wananchi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi.
 Viongozi wa tume wakizungumza na mzee Richard Kipate- Mwamotto mara baada ya tume kuwatembelea wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
 Viongozi wa tume wakizungumza na mzee Richard Kipate- Mwamotto mara baada ya tume kuwatembelea wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
 Viongozi wa tume (Hawapo pichani) wakizungumza na wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
 Viongozi wa tume (Hawapo pichani) wakizungumza na wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
Baadhi ya viongozi wa tume wakizungumza na wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
 Baadhi ya viongozi wa tume wakizungumza na wafanyabiasahara wa Soko kuu Iringa.
 Mmoja kati ya wafanyabiashara waliofanikiwa kuzungumza na viongozi wa tume, ilipotembelea soko hilo kwa lengo la kufikisha elimu ya mfumo mpya kwa jamii juu ya kuwasilisha malalamiko yao ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa tume.
 
 Nicholaus Malila mfanyabiashara mjini Iringa- akizungumza na viongozi wa tume. 
 Nicholaus Malila mfanyabiashara mjini Iringa- akizungumza na viongozi wa tume.

 Nicholaus Malila mfanyabiashara mjini Iringa- akizungumza na viongozi wa tume.
Beatrice Nkongo- mhasibu wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, wakiwa katika kikao cha utangulizi cha elimu ya ufikishaji wa malalamiko ya wananchi kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu za mkononi-"SMS". 


<<<HABARI>>>

KUKITHIRI kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, yakiwemo matukio ya uporaji wa haki za binadamu, kumeilazimu Tume ya taifa ya haki za binadamu na utawala bora, kuanzisha mkakati rahisi wa kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi.

Tume hiyo imeanzisha mpango wa kuwafikia wananchi kwa njia ya mawasiliano ya simu za mkononi kwa kupokea ujumbe mfupi, lengo likiwa ni kupunguza au  kumaliza kabisa vitendo viovu katika jamii.

Akizungumzia mpango huo Alexander Sales Hassan ambaye ni kaimu mkurugenzi wa wa elimu kwa umma na mafunzo kutoka Tume ya haki za binadamu na utawala bora amesema hatua hiyo imekuja baada ya kuona kuna changamoto ya kuwafikia wananchi.

Alexander amesema hatua hiyo ni kutokana na uwepo wa ofisi nne pekee nchini, na hivyo kundi kubwa la wananchi kushindwa kufikiwa na huduma hiyo, licha ya kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

Akitaja mikoa yenye ofisi za tume ya haki za binadamu na utawala bora, Alexander amesema ni mkoa wa Dar es salaam, Zanzibar, Mwanza na mkoa wa Lindi.

Na kuwa sasa kuna mpango wa kuanzisha ofisi katika mikoa ya Pemba, Dodoma, Mbeya na mkoa wa Kilimanjaro, na kuwa utaratibu huo mpya wa kupokea malalamiko kwa njia ya ujumbe mfupi “SMS” kutoka kwa wananchi utasaidia kuwafikia wananchi wengi.

“Changamoto zipo nyingi katika tume, lakini hili la mikoa mingi kutokuwa na ofisi zetu ni changamoto inayochangia tushindwe kuihudumia jamii kwa kiwango kinachotakiwa, lakini kupitia mpango huu mpya wa SMS kupitia njia ya simu, tutawafikia wananchi wengi zaidi,” Alisema Alexander.

Amesema kwa sasa wameanza kutoa elimu kwa njia ya ana kwa ana katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu, kama vituo vya mabasi “Stendi” Sokoni na maeneo mbalimbali ambako kuna makundi ya watu.

Wilfred Warioba ambaye ni mchambuzi mkuu wa mifumo ya habari na mawasiliano kutoka Tume amesema uelewa mdogo kwa baadhi ya wananchi ni moja ya changamoto inayoisumbua jamii kushindwa kutoa malalamiko yao.

Warioba amesema wameanza kwa kuwafikia wananchi kutumia teknolojia zilizopo zinazotumia utaalamu wa teknohama kama njia raisi kwa kutumia simu za kiganjani ikiwa pamoja na kushirikiana na taasisi zisizo za kiserikali.

Na kuwa ubunifu huo wa kwanza wa simu za mkononi zitasaidia kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati, ambapo watazishirikisha taasisi hizo zisizo za kiserikali  ambazo zitakubaliana na misingi ya tume ya kuchunguza malalamiko ya wananchi.

Alfred Machumu mchunguzi mkuu msaidizi wa Tume amesema katika baadhi ya taasisi za umma kuna changamoto ya uvunjifu wa haki za binadamu, na kuwa katika uchunguzi uliofanyika wametambua Magereza nyingi nchini zinakiuka misingi ya haki za binadamu.

Machumu amesema pia baadhi ya taasisi kuna changamoto ya rushwa, na kuwa mapendekezo yametolewa ili kuzifikia taasisi hizo ambazo zinakiuka maadili kwa kutotenda haki.

Richard Kipate mmoja wa wafanyabiashara waliopata fulsa ya kuzungumza na maafisa wa tume, amesema ipo haja kwa tume kutoa elimu kwa makundi yote, wahudumu na wahudumiwa ili elimu hiyo iwafikie wananchi wote.

Naye Baraka Kimata ameishauri Tume kushirikiana na wizara ya elimu, ili elimu hiyo ianzie shule za msingi kwa lengo la kuwajenga wananchi kuanzia hatua ya awali ya makuzi, tofauti na ilivyo sasa elimu hiyo ya haki za binadamu na utawala bora wanavyoipata ukubwani.

George Mwaitege amelalamikia hatua ya baadhi ya taasisi za umma kukithiri kwa rushwa, jambo linalowakosesha imani wananchi, katika kupata haki zao kutoka kwa watumishi wa serikali wasio waaminifu.

Hata hivyo Mwanasheria wa manispaa ya Iringa Catherine Charwe amesema katika kuifikia jamii yenye changamoto ya kutotendewa haki kutoka kwa watumishi, Manispaa imeanzisha dawati la malalamiko, ili kuboresha huduma.

“Katika kuboresha huduma kwa jamii Manispaa tumeanzisha dawati la malalamiko, lakini tatizo kubwa wananchi wetu wanapoleta malalamiko yao wanataka majibu na ufumbuzi wa masuala yao haraka, jambo ambalo haliwezekani kwani kuna mambo yanahitaji uchunguzi ili kuyapata majibu ya malalamiko hayo,” alisema Catherine.

Tume ya haki za binadamu na utawala bora inakuja na mpango huu baada ya kukwama kuwahudumia watanzania zaidi ya milioni 45, kutoka mikoa 30  yenye zaidi ya Wilaya 120 na hivyo kuamua kutumia njia hiyo rahisi ya kuwafikia wananchi, huku tatizo lingine ikiwa ni changamoto ya fedha katika kuwafikia wananchi wa maeneo yote nchini.

MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni