Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk. Retisia Warioba akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gerlad Guninita, katika kijiji cha Ilambilole (Wilaya ya Iringa)
Dr. Retisia Warioba mkuu wa Wilaya ya Iringa akifurahia kuupokea Mwenge wa Uhuru, ambao ulikimbizwa katikavijiji 13 vya Wilaya ya Iringa.
<<<HABARI>>>
WANANCHI
wa kijiji cha Isimani kilichopo Kata ya
Kihorogota – katika Wilaya ya Iringa wamefanikiwa
kujenga kiwanda cha kukamulia Alizeti chenye thamani zaidi ya shilingi Milioni
165 kwa lengo la kuepukana na adha ya kuuza zao hilo la Alizeti kwa gharama
ndogo.
Hayo yamezungumzwa na
Alfred Chakwe katibu wa kikundi cha Matumaini, wakati akitoa taarifa ya mradi
huo mara baada ya kiwanda hicho kuzinduliwa rasmi na mbio za mwenge, kama
ishara ya kubariki kazi hizo.
Chakwe amesema lengo la
mradi huo ni kuongeza thamani ya zao la Alizeti kwa kuuza mafuta badala ya
mbegu za zao hilo, kwakuwa kiwanda kitawawezesha kukamua nafaka hizo na kupata
mafuta ambayo sasa yana soko kubwa nchini.
Aidha amesema kukamilika
kwa ujenzi wa mradi huo wa kiwanda cha kukamua mafuta kumechangia na
Halmashauri ambayo imewasaidia kiasi cha shilingi Milioni 1 na laki 6 kwa
kupitia mpango wa kuendeleza kilimo Wilayani DADPs.
Amesema katika kuinua
kiwango cha zao hilo pia wamefanikiwa kujenga ghara la kuhifadhia Alizeti –
jengo lenye uwezo wa tani 400,
litakaloondoa shida ya wakulima ya kuuza kwa bei ndogo alizeti hali
iliyotokana na wakulima kukosa eneo la kuhifadhia.
Mkuu wa Wilaya ya
Iringa Dk. Retisia Warioba amesema mbio za Mwenge wa uhuru zitapita katika
vijiji 13, Kata 9 na tarafa 3 zenye umbali wa km 244, huku Mwenge huo ukizindia
jumla ya miradi 11 ya maendeleo.
Dk. Warioba amesema
thamani ya miradi hiyo ni zaidi ya shilingi milioni 585 ambayo baadhi yake
itafunguliwa, mingine itazinduliwa, itakaguliwa na mingine kuwekewa mawe ya
msingi.
Naye mkurugenzi wa
halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudensiana Kisaka amesema kati ya miradi
itakayozinduliwa na Mwenge wa uhuru ni pamoja na ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa
mradi wenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 5.
Aidha Kisaka amesema
pia mwenge utazindua nyumba bora ya wanakikundi yenye thamani ya shilingi
Milioni 9, pamoja na ujenzi wa nyumba ya mwalimu (Two in One) katika shule ya
sekondari Ilalmbilole nyumba yenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 50.
Kisaka amesema mwenge
huo utazindua daraja Nyakavangala- Mkulula lenye zaidi ya thamani ya shilingi
Milioni 151 pamoja na kukagua mradi wa madume ya Ng’ombe bora na wanyamakazi
(Maksai) mradi wenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 25.8.
Akitaja miradi mingine iliyozinduliwa
na Mwenge huo wa Uhuru ni mradi wa kikundi cha Vijana cha Ufugaji Nyuki katika
kijiji cha Ihominyi- wenye mizinga ya Nyuki 38 yenye thamani zaidi ya shilingi
milioni 3.6.
Hata hivyo Kisaka
amesema pia mbio za Mwenge huo wa Uhuru zimezindua matenki 6 ya kuvunia maji ya
mvua yenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 39.4 katika shule ya sekondari
Furahia.
Amesema Mwenge umezindua kituo cha CTC chenye thamani zaidi yashilingi
milioni 29 pamoja na mradi wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi moja ya mwalimu mkuu iliyogharimu
zaidi ya shilingi Milioni 15.9.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni