Viongozi wa kanisa la Pendekoste wakiwa katika moja ya mkutano mjini Iringa.
Sheikh Omary Nzowa- mdhamini wa Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, akizungumza na mtandao huu katika ofisi za blog hii mjini Iringa.
Mchungaji Elias Mbagata- Katibu wa umoja wa Makanisa la
Pentekoste na mratibu wa huduma ya Go and Tell, akiwa katika moja ya
mikutano yake ya awali kama ni maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika
katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
Laurens Lagerwerf- mratibu wa Go and Tell ya kanisa la Pentekoste, akiwa katika mkutano mkoani Iringa.
Mchungaji Emmanuel D. Kanemba mwenyekiti wa maandalizi ya mkutano mkuu wa Go and Tell, akizungumza na mtandao huu katika moja ya mikutano yao ya maandalizi ya mkutano mkuu- mkoani Iringa.
Mchungaji Elias Mbagata- Katibu wa umoja wa Makanisa la Pentekoste na mratibu wa huduma ya Go and Tell, akiwa katika moja ya mikutano yake ya awali kama ni maandalizi ya mkutano mkuu utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
Viongozi wa kanisa la Pendekoste wakiwa katika moja ya mkutano mjini Iringa.
Sheikh Omary Nzowa- mdhamini wa Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, akizungumza na mtandao huu katika ofisi za blog hii mjini Iringa.
<<<HABARI>>>
ZIKIWA zimepita
siku kadhaa tangu mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba BMK- Samwel Sitta kutangaza
kuwa ameteua Masheikh na Maaskofu ili kuwarejesha UKAWA Bungeni, viongozi hao
wa dini wamemtaka Sitta kuwa mkweli, muwazi na mwenye dhamira ya dhati katika kumaliza mpasuko wa bunge lake la
katiba.
Wakizungumza kwa
nyakati tofauti- katika mahojiano na Blog hii- Viongozi hao wa dini wamesema
hatua ya Sitta kuuona umuhimu wa kutafutwa suluhu kwa kuwashirikisha wao viongozi
wa dini , ni jambo la busara na sahihi ambalo litaweza kuzaa matunda, endapo tu
kiongozi huyo wa serikali Samwel Sitta atafuata kanuni na taratibu zote zinazopaswa
katika kufikia muafaka wa jambo hilo.
Mchungaji Elias
Mbagata ambaye ni katibu wa umoja wa makanisa ya Pentekoste na mratibu wa
huduma ya Go and Tell, ametoa
ushauri juu ya wazo hilo la wao viongozi wa dini kuhusishwa kuitafuta suluhu ya
mtafaruku wa wajumbe wa bunge maalumu la katiba na kuwa wenye tatizo si UKAWA
pekee, bali hata wale wajumbe wengine kuna haja ya kukaa nao kwa pamoja ili
waache kauli za kuudhi.
Mchungaji
Mbagata amesema ili kumaliza mtafaruku huo kuna umuhimu wajumbe wote
wakahusishwa katika makatazo yatakayo lenga kupatikana kwa Katiba mpya ya
Watanzania, na kuwa hakutakuwa na mafanikio endapo UKAWA pekee ndiyo wakakutana
na viongozi hao wa dini.
“Si UKAWA pekee inapaswa
wahusishwe na wajumbe wengine wote wa
bunge hilo la Katiba- tunajua katika nchi kama hakuna Katiba hakuna Amani, sisi
kama viongozi wa dini pamoja na kuomba tunalazimika kuwasihi wanasiasa kutotanguliza
maslahi yao binafsi, kwani siasa ni
muhimu - lakini watanzania ni muhimu zaidi ya siasa, yale tuliyoyaona katika
bunge la katiba lililopita hatukuyatarajia, kwani badala ya kupafanya mahala
pale sehemu ya kujadiliana na kukubaliana pakageuka ni mahali pa-kulumbana na
kushindana, na tunafahamu kuwa kadri watu wanavyolumbana wanachochea hasira,”
Alisema Mchungaji Mbagata.
Akinukuu baadhi
ya vifungu vya biblia mchungaji Mbagata amesema “katika kitabu cha Mithali 15: 1 unasema Jawabu la upole hugeuza
hasira bali neno liumizalo huchochea ghadhabu- … tunamshukuru sana rais Kikwete
kwa hekima aliyonayo nakwa busara nakwa mwongozo alioutumia kuteua wajumbe wakujadili
mchakato wa katiba mpya– ni jambo zuri sana, lakini yale tuliyoyaona katika
bunge lililopita wengi yalituumiza sana mioyo-
cha msingi wale wote waliopewa dhamana hiyo na Rais ya kujadili mchakato wa
Katiba mpya wakubali kuwa pamoja, wawe ni
UKAWA au wajumbe wengine wazungumze kwa upole nasi kwa hasira, hapo hawatafikia
muafaka, kwani wasipofikia muafaka amani itavunjika, “Alisema mchungaji
Mbagata.
Pia aliwataka wajumbe
watambue kuwa wenye dhamana ya kuipigia kura rasimu hiyo kwa kuikubari au
kuikataa ni wananchi na si wanasiasa ambao wanaendelea na malumbano, kwani sasa
wote kwa pamoja wanapaswa kukubaliana ili kufikia muafaka wa kuipata Katiba
mpya.
“UKAWA ni muhimu
wakarudi bungeni lakini na hawa wengine wanapaswa kuwa na Lugha ambazo haziwezi kuwaumiza wenzao
ili pande zote mbili waweze kwenda pamoja, lakini hoja si kuongea na UKAWA peke
yao wahusishwe pamoja na hao wengine,” Alisema mchungaji Mbagata.
Alimtaka rais
asichoke, asikate tamaa kwa hekima na busara aliyonayo na badala yake atafute
kila namna ili aweze kuwaita UKAWA waweze kukubaliana kwa kutumia nafasi
aliyonayo kwa lengo la kunusuru mchakato mzima wa upatikanaji wa Katiba mpya.
Naye Sheikhe
Omary Nzowa ambaye ni mdhamini wa baraza la Waislamu BAKWATA Taifa akirejea
kauli ya Mwenyekiti wa bunge maalumu la Katiba Samwel Sitta – ya kutaka kuwaita
viongozi wa dini kukutana na kamati ya
mashauriano july 24 - ili kusaidia suluhu ya utata na tofauti zilizopo- Nzowa
amesema Samwel Sitta anatakiwa kuwa mkweli na muwazi ili suluhu ipatikane.
Sheikh Nzowa
amemtaka mwenyekiti huyo wa Bunge
Maalumu la Katiba BMK kuwa na dhamira ya kweli pasipo kuficha mambo ili
kufikia muafaka wa mpasuko wa bunge lake, kwa madai kuwa ukweli ndiyo silaha ya
muafaka katika tatizo hilo.
Aidha Sheikh
Nzowa amesema mwenyekiti huyo anatambua wazi chanzo cha tatizo la UKAWA
kuondoka bungeni, kwani kuna masuala ambayo yaliwakera wajumbe hao, na sasa ipo
haja ya kutafuta suluhu kwa msaada wa Mungu kwani jambo hilo ni nito
linastahili viongozi wa dini kuhusishwa.
Nzowa amesema
kwa maoni yake anaona mwenyekiti huyo wa BMK ana dhamana kubwa kuona mtafaruku
hautokei tena katika bunge lake, na kuwa wazo la Sitta linaweza kuleta suluhu,
kwani inapotokea watu wawili wakazozani ni lazima akatokea mtu wa tatu mwenye
nguvu ya kusikilizwa ili kutambua nani amekosea na kumaliza utata uliopo.
Amesema sababu
kubwa ya viongozi wa dini kuwa na nguvu ya kumaliza tofauti ni kutokana na
wanachama wote wa vyama vya siasa kuwa waumini wa dini- nakwa hali hiyo
viongozi wa dini wanaweza kuwakutanisha na kufikia muafaka wa suala hilo, hasa
suala la Ukweli likitangulizwa mbele.
“Matumaini yangu
ni kuwa viongozi wa dini wanastahili na kama Samwel Sitta ameamua kwa nia thabiti
kuwaita viongozi wa dini kwa maana ya kumsaidia kutatua mfarakano huo jambo
hilo litafanikiwa, kwani viongozi wa dini wanazijua dhamana zao- lakini pia
wanamuogopa Mwenyezi Mungu, matumaini yake mambo yatakwenda vizuri, lakini kama
ukweli hautakuwepo hiyo ni kazi bure, kwani kwa ujanja ujanja haiwezi
kupatikana suluhu kwani kwenye ukweli kuna msaada wa Mungu,” Alisema Nzowa.
“………Kwanza nimsihi
mwenyekiti kuwa aliipata dhamana kubwa na anayo dhamana kubwa kwa Watanzania, na
sisi viongozi wa dini tunapoona machafuko na mgongano tunajua nini kitatokea
baadaye, nchi yetu hii ni nchi ya amani lakini ukitokea mfarakano mmoja wa watu
watakaosononeka ni pamoja na mimi,” alisema.
Hata hivyo July
16 2014 Kanisa la Pentekoste nchini linataraji kufanya mkutano wa kuliombea
Taifa ili liepukana na matukio mbalimbali yasiyo ya kawaida, – mkutano
utakaofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Wilolesi mjini Iringa.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni