Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dr. Retisia Warioba akiwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wakati wakijadili suala la mgogolo wa wafugaji na wakulima wilayani humo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa- akizungumzia mgogolo huo wa wakulima na wafugaji katika kikao cha baraza la madiwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Pedensiana Kisaka akiwa katika kikao hicho cha baraza la madiwani, kilichojadili masuala mbalimbali likiwemo jambo la mgogolo wa wakulima na wafugaji.
Makamu mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Costantino Kihwele- akisikiliza jambo katika kikao cha baraza la madiwani.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya iringa Steven Mhapa. akifafanua jambo.
Kushoto ni mkuu wa Wilaya Dr. Retisia Warioba akiwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya iringa wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani ambacho kimetolewa taarifa ya baadhi ya viongozi kushikiliwa na TAKUKURU.
<<<HABARI>>>
BAADHI ya
viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa, wametupiwa lawama kwa kujihusisha kugombanisha
baina ya kundi la wakulima na wafugaji, na hivyo kusababisha maisha yao kuwa
hatarini.
Hayo
yamezungumzwa katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya
Iringa – wakati wakijadili masauala mbalimbali ya amendeleo na changamoto
zinazowakabili, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa “Siasa ni Kilimo” mjini
Iringa.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema wamebaini uwepo wa baadhi
ya viongozi kupokea rushwa kwa kundi la wafugaji kutoka nje ya mkoa wa Iringa,
na kisha kuwaruhusu wafugaji hao kuingiza mifuho jambo linalozua migogoro ya hatari ya mara kwa
mara.
Mhapa amesema
kukithiri kwa tabia hiyo hasa kwa baadhi ya viongozi katika Tarafa ya Pawaga
kumekuwa kukisababisha viongozi ngazi ya Wilaya kutofanya kazi kwa kushindia kutatua migogolo hiy.
“Kwa kweli kule Pawaga
kuna matatizo ambayo tunaimba serikali ifanye juhudi za maksudi na haraka kutatua
tatizo, kwani kuna uvamizi unaotoka nje ya Wilaya, uvamizi huu unafanywa na
wafugaji, ambaop wana nnakuna viongozi wengine tumepata taarifa kuwa
wanajishughulisha na rushwa, wale wafugaji wanakuja na fedha wanawapa viongozi
na viongozi wanawaruhusu wafugaji kuingiza mifugo yao, viongozi hao lazima wachukuliwe hatua kali
sana za kisheria,” Alisema.
Amesema ili
kuondokana na tatizo hilo la mgogolo Halmashauri yake imemejipanga kufanya sensa
ya mifugo katika Wilaya hiyo lengo likiwa ni kutambua idadi ya wafugaji na
kuwawezesha kutambua eneo watakalotenga
kwa ajili ya malisho.
Mhapa amesema wilaya
yao ni ndogo na kuwa hawahitaji wavamizi wowote wala mifugo kutoka nje - na kuwa
mgogolo huo zaidi upo Kata ya Itunundu, na suluhu ya tatizo hilo katika
kuepusha mauaji ni kuchukuliwa maeneo ya zamani ya wachungaji ili kusaidia
kupunguza tatizo hilo.
Amesema tayari
wameandika barua kwa Waziri mwenye dhamana ikiwa pamoja na nakala kuifikisha
katika ofisi ya Waziri mkuu ili kuifahamisha serikali juu ya hatari iliyopo
katika Halmashauri yao.
Diwani wa Kata
ya Itunundu Halfani Lulimi amesema mgogolo huo ambao unaigusa na kata yake,
unachangia maendeleo kudhorota, kwa kuwa kuna wakati vurugu hizo zilitaka
kusababisha maafa ambapo hata askari polisi alitaka kuuawa katika vurugu hizo.
“Kuna tatizo
kubwa sana hasa kule kule kwenye Kata ya Mlengo na Itunundu, na mwingiliano huo
niwa maeneo ya machungo na kilimo, hasa msimu wa kilimo Kata ya Itunundu na
Mlenge zinazoingiliana katika matumizi ya miundombinu ya kilimo,” alisema
Lulimi.
Amesema madhara
ambayo tayari yametokea ni pamoja na wananchi kupigwa huku askari wakitishiwa
kuuawa, mara tu unapozuka mgogolo huo.
Diwani Lulimi
amesema awali aliishauri serikali kutoa eneo la “Lunda Kaskazini Mkwambe” ili
wafugaji wakakae huko, na kuwaachia wakulima eneo lenye mgogolo, na kuwa hilo
litakuwa ni suluhu ya mgogolo huo- kwani kiini cha mapigano ni mwingiliano wa
maeneo ya kilimo na mifugo.
Mkuu wa Wilaya
ya Iringa Dr. Retisia Warioba amesema viongozi wanaosababisha wakulima na
wafugaji kuingia katika mgogolo ambao umedumu kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, tayari
wanashilikiwa na taasisi ya kudhibiti na kuzuia Rushwa TAKUKURU.
Dr. Warioba
amesema migogolo iliyopo katika kata za Pawaga niya hatari hasa katika Kata ya Magozi
ambapo wafugaji huchungia mifugo kwenye mashamba ya wenzao, na kuwa kila mwezi kamati
ya ulinzi na usalama wanakwenda mara tatu Pawaga kutatua mgogolo huo.
Dr. Warioba
amesema wahusika wa matukio ya kupokea fedha wametajwa na wafugaji kuwa ni Mtendaji na mwenyekiti ambao sasa
wamekabidhiwa mikononi mwa TAKUKURU, na kuwa wamefanya doria kubwa ya kuwaondoa
wavamizi wote.
Kwa mujibu wa
bajeti ya mwaka 2013/2014 Tanzania inakadiliwa kuwa na zaidi ya ng’ombe zaidi ya milioni 22, mbuzi zaidi ya
milioni 15, Kondoo zaidi ya milioni 7 na Nguruwe zaidi ya milioni 2, ambapo
Wizara husika imezitaka Halmashauri kuandaa Mipango ya Matumizi ya Ardhi na
kutenga maeneo ya ufugaji, kwa ajili ya kuendeleza malisho ya mifugo ili kuepusha
migogoro ya mara kwa mara .
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni