Jumapili, 12 Oktoba 2014

TIGO YAZINDUA HUDUMA MPYA


 Basi jipya la Kisasa – liitwalo “Experience Zone” ambalo linataraji kuanza kutoa huduma kwa kuwafikia wateja katika mikoa yote nchini.
 “Experience Zone” likiwa tayari limezinduliwa rasmi kwa kuanza kazi ya kuwafikia watanzania ili kuwapatia huduma ya kidigitali.
Jackson Kiswaga- Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo Nyanda za juu Kusini, akifafanua jambo kuhusiana na huduma hiyo mpya.
 Dr. Christine Ishengoma- Mkuu wa mkoa wa Iringa, akitoa hotuba katika uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo, katika uwanja wa samora mjini Iringa.
 Jackson Kiswaga.


<<<HABARI>>>


KAMPUNI ya mtandao wa Simu za mkononi ya TIGO imezindua huduma mpya ya kifurushi cha “WELLCOM PARK” Kifurushi chenye lengo la kuwakaribisha wateja wapya wanaojiunga na mtandao huo wa Tigo.

Hayo yamezungumzwa na Jackson Kiswaga, Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo nyanda za juu kusini, wakati akitoa taarifa juu ya mafanikio ya kampuni yake na mikakati ya kuwafikia watanzania walio wengi.

Uzinduzi huo ambao umefanyika katika uwanja wa Samora mjini Iringa, umehudhiriwa na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dr. Christine Ishengoma ambaye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo, Katibu Tawala mkoa wa Iringa Wamoja Ayub, Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi.

Kiswaga amesema mpango huo utawashawishi wateja wengi kujiunga na Tigo, kwani utaambatana na fulsa ya kuwafundisha wateja elimu ya Digitali kwa kutumia Simu zao za mikononi.

Aidha Kiswaga amesema kwa kutumia Basi jipya la Kisasa – liitwalo “Experience Zone” wataweza kuwafikia watanzania walio wengi nchi nzima kwani gari hilo lina huduma ya mtandao  wa masafa marefu  wa Internet, ambapo huduma kama ya U-Tube, Whatsap , Twiter na huduma mbalimbali zinazohusiana na Internet zitafanyika katika Basi hilo.

Katika uzinduzi huo pia wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa ndani ya mkoa wa Iringa na nje ya  Iringa walipanda jukwaa kusherehesha uzinduzi huo, huku wasanii wa sanaa ya maigizo kutoka kikundi cha Comed ..Joti, Wakuvwanga nk. Walikuwepo.

MWISHO


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni