Baadhi ya wenyeviti wa Kata ya Kitwiru - Manispaa ya Iringa wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Iringa - Angelina Mabula alipotembelea ujenzi wa maabara ya shule ya sekondari Ipogolo- iliyopo Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa.
DC- Angelina Mabula akizungumza na baadhi ya viongozi wa Manispaa ya Iringa.Baadhi ya wenyeviti wa mitaa ya Kata ya Kitwiru - mjini Iringa - wakimsikiliza kwa makini mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula.
Baadhi ya wenyeviti wa mitaa iliyopo katika Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Iringa wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Iringa- Angelina mabula.
DC- Mabula akihimiza jambo katika ziara yake ya kikazi ya kuhimiza ujenzi wa Maabara katika shule za sekondari za Manispaa ya Iringa.
<<<<HABARI>>>>>.
MKUU
wa Wilaya ya Iringa - Angelina Mabula amewataka viongozi wa serikali kuwa mfano katika uchangiaji wa fedha za ujenzi wa maabara ya Sayansi- lengo likiwa ni kufanikisha mpango huo kwa wakati pasipo kuwaachia wananchi shughuli hiyo pekeyao.
Mabula ameyasema hayo wakati akikagua ujenzi wa maabara za Sayansi katika shule za sekondari za Manispaa ya Iringa, ziara ya kikazi ambayo pamoja na mambo mengine Mabula alianzisha harambee ya fedha za ujenzi wa maabara ya shule hiyo ya sekondari Ipogolo- ujenzi uliokuwa umesimama kutokana na mkwamo wa kifedha.
Aidha Mabula amewataka viongozi wa mitaa, vijiji na vitongoji kuachana na masuala ya siasa kwenye mambo ya msingi yenye mlengo wa kujenga Taifa, ukiwemo ujenzi huo wa maabara- na hiyo ni kutokana na baadhi ya wenyeviti hao kutuhumiwa kuwazuia wananchi kutoa michango.
Mabula amesema kuna umuhimu sasa viongozi wakajielekeza kwa nguvu zote katika shughuli za maendeleo - huku wao wakiwa mstari wa mbele katika utoaji wa michango ili kuleta chachu kwa jamii katika kutekeleza masuala ya maendeleo.
Aidha Mabula ameanzisha mchango wa fedha za ujenzi wa maabara ya Sayansi kwa shule ya sekondari, huku akiwahimiza wenyeviti wa mitaa wa Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa kuwa mstari wa mbele katika zoezi hilo ili wananchi waweze kulipokea kwa mikono miwili.
Harambee hiyo imezaa matunda baada ya wenyeviti wa Kata ya Kitwiru na baadhi ya wataalamu walioongozana na mkuu huyo kuchangia zaidi ya shilingi laki nne ambazo zitafanikisha ujenzi wa Maabara hiyo kuendelea.
Mpango huo wa Mkuu wa Wilaya Mabula unadaiwa kuwa unaweza kutoa majawabu ya kukwama kwa ujenzi mbalimbali wa Mabaara katika shule za Sekondari.
Hata hivyo mkuu huyo Mabula ameahidi kuchangia mifuko mitano ya Saruji kwa shule hiyo ya Sekondari Ipogolo, lengo likiwa ni kukamilisha ujenzi huo wa Maabara itakayowawezesha wanafunzi kujifunza kwa Vitendo masomo ya Sayansi ambayo kwa sasa baadhi ya walimu wanalazimika kuyafundisha kwa nadharia badala ya Vitendo.
MWISHO.
MWISHO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni