Baadhi ya wananchi wa Nyamuhanga- katika Kata ya Kitwiru Manispaa ya Iringa, wakiwa katika mkutano wa dharula wakijadili uuzwaji wa kiwanja ambacho kilitakiwa kujengwa shule ya sekondari.
Baadhi ya wakazi wa Nyamuhanga kisikiliza jambo kwa makini.
Baadhi ya viongozi wa Kata ya Kitwiru na watumishi wa Manispaa ya Iringa wakiwa katika mkutano huo wa mgogoro wa ardhi iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari.. inayodaiwa kuuzwa na Manispaa kwa watu binafsi.
<<<HABARI>>>
WANANCHI wa
Nyamuhanga na mitaa iliyopo katika Kata ya Kitwiru mjini Iringa – wameitupia lawama Manispaa ya
Iringa kwa kuuza eneo la kiwanja –
lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari, kiwanja kilichotolewa
na mmoja wa wananchi wa eneo hilo.
Mgogolo huo umezuka baada ya awali wananchi
hao kudai kuchangia nguvu kazi pamoja na fedha, kwa ajili ya ujenzi wa shule yao ya
sekondari katika kiwanja hicho, nguvu kazi ambazo zilielekezwa kwenye ujenzi wa
shule ya sekondari Ipogolo.
Wakizungumza
katika mkutano wa dharula uliofanyika katika eneo la Pipe line Nyamuhanga- mjini
Iringa, wananchi hao wamesema ujenzi wa shule hiyo ulipaswa kuanza mwaka 2012
na ungekuwa umekamilika, lakini umecheleweshwa na maamuzi ya baadhi ya viongozi
wa Kata na Manispaa ya Iringa.
Emmanuel Kabongo
mjumbe wa mtaa wa Nyamuahanga “C” amesema katika eneo lililotakiwa kujengwa shule, tayari kuna nyumba imejengwa,
na hivyo kuwataka viongozi kufuatilia jambo hilo ili kuwapunguzia adha umbali ya kutembea umbali mrefu wanafunzi - kwenda katika shule ya sekondari Ipogolo.
Janeth Myovela mmoja
wa watoto wa mwananchi aliyetoa ardhi hiyo ambayo inatakiwa ijengwa shule, amesema
ameshangazwa na taarifa za kuwa baba yake “George Myovela” kuwa anamgogolo wa
ukoo juu ya kiwanja hicho, kwani baba yake alitoa ardhi hiyo na kuipa jina
shule kuwa itaitwa Temihanga Sekondari jina la baba yake na George Myovela.
“Mimi kwa kweli
hapa ninashangaa kusikia eti kiwanja hiki kinamgogolo wa kiukoo, hili ndiyo
ninalisikia leo, baba yangu alitoa eneo hilo ili ijengwe shule huku akitoa na mawe
ili shule itakayojengwa iitwe jina la marehemu baba yake, yaani babu yetu mzee
Temihanga,.. mimi kama mtoto wa mzee George Myovela hilo jambo la ugomvi wa
kiwanja sijawahi kulisikia au mnamzushia kwa vile baba anaumwa!!?, Alisema
Janeth.
Bahati Chaula
mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyamuhanga “B” amesema mkutano huo umekuja
baada ya wananchi kusikia kuwa eneo walilopewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari
kuna jengo la nyumba huku ujenzi mwingine ukiendelea.
Peter Siwa
Mwenyekiti wa mtaa wa Kisiwani, amesema kiwanja hicho walipewa mnamo mwaka
2010, ambapo walianza kukusanya mawe na nguvukazi mbalimbali kwa ajili ya
ujenzi wa shule ya sekondari, lakini walipewa taarifa ya kuhamishwa kwa mawe na
kupelekwa eneo la Kitwiru katika ujenzi wa shule ya sekondari Ipogolo.
Siwa amesema baada
ya kuhoji utaratibu uo wa uhamishaji wa nguvu kazi zao, waliambiwa na viongozi kuwa
baada ya kukamilika kwa ujenzi wa sekondari ya Ipogolo, wangeelekeza nguvu ya
pamoja katika ujenzi wa shule katika eneo hlo la Nyamuhanga, na sasa
wameshtushwa kuona eneo hilo linaendelezwa ujenzi wa nyumba za watu binafsi.
Baraka Kimata
mwenyekiti wa mtaa wa Nyamuhanga .. amesema kukosekana kwa shule katika eneo
hilo kutasababisha wanafunzi kukosa baadhi ya masomo kwani eneo hilo halina
shule na hivyo wanafunzi hulazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 5 kuifuata
elimu katika sekondari ya Ipogolo na ..
Kimata amesema
licha ya kukosekana kwa shule pia eneo la Nyamuhanga halina huduma za msingi
kama Zahanati, Kituo cha Polisi, Soko wala shule ya watoto wadogo - licha ya
kutokuwepo kwa maeneo ya wazi.
Aidha Kimata
amesema kama ujenzi huo ungekuwa umeanza mapema shule hiyo ingekuwa
imeanza kutoa wanafunzi wa kidato cha nne mara tatu, lakini mpaka sasa kiwanja
hicho hakina kitu chochote zaidi ya majengo yanayoanza kujengwa na watu binafsi.
Wananchi hao
wamesema kamwe hawatakuwa tayari kuchangia michango yoyote ya shughuli za maendeleo,
kwani michango mingi waliyotoa haina tija kwao, kwa kuwa imekuwa ikichangia maendeleo
katika maeneo mengine na wao wakiendelea kupata taabu ya kuzifikia huduma
muhimu za kijamii.
Erneus Kivili
mkazi wa Kitwiru, amesema haoni kama kuna uhalali wa kuendelea kuchangia ujenzi
mwingine katika shule ya sekondari Ipogolo kwani awali waliambiwa baada ya
kujenga majengo matatu ya shule ya Ipogolo– nguvu ya wananchi wote ingehamia katika ujenzi wa shule
eneo la Nyamuhanga jambo ambalo kwa zaidi ya miaka 8 sasa halijaanza.
Kivili amesema kumekuwa
na michango mbalimbali juu ya ujenzi wa maabara katika shule ya Sekondari ya
Ipogolo – michango ambayo inawachanganya, kutokana na ujenzi wa shule yao kutopewa kipaumbele.
Hata hivyo
wananchi hao wamesema wamepata tetesi za kuwa Kata ya Kitwiru itagawanyika, na kuwa Kata mbili tofauti, jambo ambalo
litakuwa ni hasara kwao wakazi wa Nyamuhanga- kwani michango yao mingi imeelekezwa upande wa eneo
litakalokuwa Kata nyingine na hivyo wao kubaki hawana shule, Soko, wala kituo
cha afya.
Afisa ardhi wa Manispaa
ya Iringa Wicklif Benda amesema manispaa haijauza viwanja katika eneo hilo, na
sababu za kutojengwa shule katika kiwanja hicho ni kukosekana kwa vigezo kikiwemo
cha kiwanja kutolipiwa fidia, kukosa mchoro
wa mipango miji na pia eneo hilo lina mgogolo wa kifamilia.
Naye Charles
Lawiso Mwanasheria wa Manispaa ya Iringa
amesema mgogolo huo utaundiwa timu ya kamati ndogo ya wataalamu ili kutafuta
suluhu, na kuwataka wananchi kuwa na subira mpaka kamati itakapotoa majawabu ya
nini kifanyike.
MWISHO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni