Jumanne, 10 Machi 2015

IRINGA KIBIKI CHILDREN CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI IRINGA

 MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI

MRATIBU WA KIBIKI CUP HARUNA SALEH AKIWA NA MDAU WA SOKA FRANK KIBIKI na wanahabari
 
NA MWANDISHI WETU, IRINGA
 
LIGI inayoshirikisha  watoto walio chini ya umri wa miaka 16, inaloitwa  Iringa Kibiki Childrens Cup 2015 yenye lengo la kupinga mauaji ya walemavu wa ngozi (Albino) inatarajia kuanza kutimua vumbi jumamosi ikishirikisha timu nane za manispaa ya Iringa.
 
Mratibu wa ligi hiyo, Haruna Salehe alisema lengo la mpira huo ni kukuza vipaji vya watoto na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili na mauaji yanayofanywa kwa walemavu wa ngozi nchini.
 
Alisema ligi hiyo iliyobuniwa na kuendeshwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru, inatarajia kushirikisha timu nane za watoto katika manispaa ya Iringa.
 
“Lengo kubwa ni kukuza vipaji na kueneza ujumbe wa kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wenzetu walemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiuawa kila siku bila huruma jambo ambalo, hatutaki liendelee kwenye jamii yetu,”alisema
 
Alisema michuano hiyo itakuwa ikifanyika katika uwanja wa mwembetogwa ambao ni wa wazi ili watu wengi wapate nafasi ya kushiriki.
 
Kwa upande wake, mdau wa soka na mwanahabari wa gazeti hilo, Frank Kibiki alisema ameamua kubuni ligi hoyo ili kupanda mbegu ya kupenda michezo na kutambua vipaji vya soka tangu utotoni, ili iwe rahisi kuwapata wachezaji bora siku zijzo.
 
“Mpira ni ajira na huu hauna dini, kabira wala rangi, watu wote hata watoto wanaweza kushiriki kwenye mpira hivyo tumebuni jambo hili ili kuendelea kukuza vipaji huku tukibeba ujumbe wa kupinga ukatili kwa wenzetu wenye ulemavu wa ngozi,”alisema
 
Kibiki ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa soka kushiriki kwenye michuano hiyo ili kusaidia kuibua vipaji na kulifanya soka la Iringa kuwa endelevu.
 
Alisema tayari shirikisho la Soka, manispaa ya Iringa wametoa Baraka za kuanza kwa ligi hilo, ambalo watoto wameshaewa mafunzo ya kuwa waamuzi na washika vibendera hiyo wao wenyewe watajiongoza.
 
Kwa upande wao wadau wa soka, manispaa y
aa Iringa waliitaka serika kutambua mchango na kuwekeza kwenye soka ili kusaidia kupandisha timu zilizopo na kuendelea kuibu vipaji ikiwemo michuano ya watoto.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni